Wananchi zaidi ya 18,000 wanatarajiwa kunufaika na huduma za usalama kupitia Kituo kipya cha Polisi Isaka, kilichojengwa katika Kata ya Isaka, Halmashauri ya Msalala, Mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Janeth Magomi, ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na wananchi katika kufanikisha ujenzi wa kituo hicho.
Kamanda Magomi amesema Jeshi la Polisi litapeleka askari wa kutosha katika kituo hicho ili kuhakikisha huduma zinapatikana wakati wote, akieleza kuwa Mji wa Isaka unaendelea kukua kutokana na uwepo wa Bandari Kavu.
Aidha, amewataka askari kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni zinazowaongoza katika utendaji kazi.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Msalala, Mhe. Mabula Magangila, amempongeza Kamanda Magomi kwa juhudi za kudumisha amani na utulivu mkoani Shinyanga.
Amesema kuimarika kwa Polisi Jamii kumesaidia kubadilisha mtazamo wa vituo vya Polisi kuwa maeneo ya kutoa huduma, malezi na kuzuia uhalifu kabla haujatokea. Mhe. Magangila amesema anatamani kuona utamaduni huo ukiendelea na kutawala katika vituo vyote vya Polisi.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment