" MWENYEKITI UVCCM MISSENYI ACHA ALAMA KILIMILILE, ATOA KOMPYUTA ZA MILIONI 1.4

MWENYEKITI UVCCM MISSENYI ACHA ALAMA KILIMILILE, ATOA KOMPYUTA ZA MILIONI 1.4

Na Avitus Benedicto - Misalaba Media

MISSENYI/KAGERA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Missenyi, Mkoa wa Kagera,  Kelvin Paschal Nazar, ametoa kompyuta mbili zenye thamani ya shilingi milioni 1.4 kwa Shule ya Sekondari Kilimilile, iliyopo Kata ya Kilimilile, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.

Akikabidhi msaada huo wakati wa mahafali ya 18 ya shule hiyo, Kelvin amesema ameamua kutoa kompyuta hizo baada ya kubaini changamoto ya upungufu wa vifaa hivyo iliyowasilishwa na wahitimu kupitia risala yao, hatua iliyomsukuma kuchukua hatua ya kusaidia shule hiyo.

Amesema elimu ni msingi muhimu wa maendeleo ya mtu binafsi na Taifa kwa ujumla, hivyo amewataka viongozi na wadau mbalimbali kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha mazingira ya elimu ili wanafunzi wapate fursa nzuri ya kujifunza na kutimiza malengo yao.

Aidha, amewataka wazazi na walezi kuwaunga mkono watoto wao waliomaliza elimu ya sekondari kwa kuwawezesha kuendelea na masomo ya elimu ya juu katika vyuo mbalimbali, ili wapate maarifa na ujuzi utakaowasaidia kujitegemea na kushiriki katika shughuli za maendeleo ya Taifa.

Vilevile, amewahimiza wahitimu hao kuwa wazalendo, kuthamini na kulinda amani ya nchi pamoja na kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuhatarisha utulivu wa jamii, akisisitiza kuwa amani ni nguzo muhimu katika kufanikisha maendeleo ya Taifa.

PROFESSOR MGOKO EPISODE 07

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post