Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Katavi na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa huo, Ndg. Evarist Simon Mnyere, akiunga mkono juhudi zinazoendelea kufanyika kuhakikisha eneo la Shule ya Sekondari na Ufundi Milala, iliyopo Kata ya Misunkumilo, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, linapimwa na kupatiwa hati miliki. Hatua hiyo ni sehemu ya mikakati ya kurejesha shule hiyo katika hali ya kutoa mafunzo ya sekondari na ufundi kupitia eneo linalomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda.
Kamati ya
Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda imefanya kikao maalumu
cha tathmini ya maendeleo ya juhudi za kufufua Shule ya Sekondari na Ufundi
Milala iliyopo Kata ya Misunkumilo, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, mkoani
Katavi, ambayo kwa mujibu wa taarifa zilizowasilishwa katika kikao hicho
haijafanya kazi kwa zaidi ya miaka mitano.
Kikao hicho
kilichofanyika Oktoba 29, 2026, kimeongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi
CCM Wilaya ya Mpanda, Ndg. Pius M. Buzumalle, ambapo pamoja na mambo mengine,
wajumbe wamejadili hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kurejesha shughuli za
shule hiyo na kuiwezesha kutoa elimu ya sekondari na mafunzo ya ufundi kwa
vijana.
Katika
majadiliano hayo, wajumbe wameeleza umuhimu wa kufanya tathmini ya hali ya
shule, kuboresha miundombinu na kupanga eneo lake ili kuweka mazingira
yatakayowezesha kurejesha shughuli za utoaji wa elimu na mafunzo ya ufundi.
Mojawapo ya
changamoto zilizobainishwa ni kutokuwepo kwa hati miliki ya eneo la shule hiyo,
hali ambayo imeelezwa kuhitaji hatua za haraka ili kuhakikisha umiliki wa eneo
unalindwa na mali ya Jumuiya ya Wazazi inakuwa salama.
Wajumbe pia
wameeleza kuwa miongoni mwa mahitaji muhimu katika hatua za kufufua shule hiyo
ni fedha kiasi cha Shilingi milioni 2.333 kwa ajili ya upimaji na upangaji wa
eneo. Aidha, wameeleza umuhimu wa mshikamano na ushirikiano wa pamoja katika
kutafuta suluhisho la changamoto zinazoikabili shule hiyo.
Kutokana na
hali hiyo, Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda imetoa wito kwa wadau
mbalimbali wenye nia ya kusaidia maendeleo ya elimu kujitokeza kushirikiana
katika upimaji wa eneo, uboreshaji wa miundombinu na mazingira ya shule hiyo.
Katika hatua
nyingine, kikao hicho kimejadili mikakati ya kuimarisha uhai wa Jumuiya ya
Wazazi kupitia kuongeza idadi ya wanachama, kuhamasisha ulipaji wa ada za
uanachama kwa wakati na kuongeza ushiriki wa wanachama katika shughuli za
jumuiya.
Ili
kutekeleza mikakati hiyo, maafisa wa jumuiya kwa kushirikiana na maafisa wa
TEHAMA wamepangwa kutembelea matawi na kata, huku zoezi la uandikishaji
likitarajiwa kufanyika kwa utaratibu wa duka kwa duka na nyumba kwa nyumba ili
kutoa elimu kuhusu uanachama na mifumo ya usajili.
Vilevile,
wajumbe wamejadili umuhimu wa kuanzisha na kuimarisha miradi ya kiuchumi katika
ngazi za matawi na kata ili kuongeza mapato ya jumuiya na kupunguza utegemezi
wa michango katika kugharamia shughuli zake.
Kikao hicho pia kimesisitiza umuhimu wa viongozi kutembelea matawi na kata kwa ajili ya kutoa elimu kwa wanachama na wananchi kuhusu masuala ya malezi, elimu, mazingira, afya na utamaduni, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya Jumuiya ya Wazazi katika Wilaya ya Mpanda.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Ndg. Pius M. Buzumalle, akiongoza kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, kilichofanyika Oktoba 29, 2026.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akishiriki kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, kilichofanyika Oktoba 29, 2026, kwa lengo la kujadili mikakati ya maendeleo na ufufuaji wa Shule ya Sekondari na Ufundi Milala.

Majengo, madarasa na uwanja wa Shule ya Sekondari na Ufundi Milala, iliyopo Kijiji cha Milala, Kata ya Misunkumilo, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Mkoa wa Katavi. Kupitia kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda kilichofanyika Oktoba 29, 2026, wadau mbalimbali wenye mapenzi mema na shule hiyo wameombwa kujitokeza kuchangia hali na mali ili kuwezesha eneo la shule kupimwa na kupatiwa hati miliki. Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kurejesha shule katika hali yake ya awali ya kutoa mafunzo na kuwezesha vijana kunufaika na elimu kupitia eneo hilo.

Majengo, madarasa na uwanja wa Shule ya Sekondari na Ufundi Milala, iliyopo Kijiji cha Milala, Kata ya Misunkumilo, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Mkoa wa Katavi. Kupitia kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda kilichofanyika Oktoba 29, 2026, wadau mbalimbali wenye mapenzi mema na shule hiyo wameombwa kujitokeza kuchangia hali na mali ili kuwezesha eneo la shule kupimwa na kupatiwa hati miliki. Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kurejesha shule katika hali yake ya awali ya kutoa mafunzo na kuwezesha vijana kunufaika na elimu kupitia eneo hilo.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akiwa ofisini akifanya maandalizi ya kikao maalumu cha Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya hiyo kilichofanyika Oktoba 29, 2026, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda.

Mjumbe wa Kamati Ndogo ya Uchumi, Mipango na Fedha ya Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Heliuth Henry Mbilinyi maarufu kama Makete, akichangia shilingi 500,000 kwa ajili ya kugharamia upimaji wa eneo la Shule ya Sekondari na Ufundi Milala, iliyopo Kijiji cha Milala, Kata ya Misunkumilo, ili shule hiyo iweze kupatiwa hati miliki. Pia amewahimiza wadau wengine kujitokeza kuunga mkono juhudi za kufanikisha hatua hiyo kwa manufaa ya vijana wa sasa na vizazi vijavyo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Ndg. Pius M. Buzumalle, akiwa katika kikao maalumu cha Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya hiyo, akifanya mawasiliano na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Katavi, Ndg. Evarist Simon Mnyere, kuhusu mipango na mikakati ya kufufua na kuendeleza Shule ya Sekondari na Ufundi Milala.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Ndg. Pius M. Buzumalle, akiwa katika kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, kilichofanyika Oktoba 29, 2026.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Ndg. Frank William Mgata, akishiriki kikao maalumu cha kamati hiyo kilichofanyika Oktoba 29, 2026.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Ndg. Plasido Peter Kameme, akishiriki kikao maalumu cha kamati hiyo kilichofanyika Oktoba 29, 2026.
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda wakiwa katika kikao maalumu cha kamati hiyo kilichofanyika Oktoba 29, 2026.PROFESSOR MGOKO EPISODE 07
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




























Post a Comment