Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Jimotoli Jilala Maduka, ameendelea na zoezi
la kutembelea maduka ya wafanyabiashara katika Mji wa Mpanda kwa lengo la
kuandikisha wanachama wapya wa CCM na Jumuiya ya Wazazi.
Zoezi hilo lililofanyika Oktoba 28, 2026, limewezesha
kuandikishwa kwa wanachama wapya tisa, ambapo wote wamelipa ada ya uanachama
yenye jumla ya Shilingi 17,900.
Wakati wa ziara hiyo, Maduka alitembelea baadhi ya maduka ya
wafanyabiashara, akizungumza nao kuhusu uanachama wa CCM na Jumuiya ya Wazazi,
huku akiwapatia kadi za Umoja wa Wazazi wa Tanzania wale waliojiandikisha
kupitia jumuiya hiyo.
Alisema utaratibu wa kuwafikia wafanyabiashara katika maeneo
yao ya kazi ni miongoni mwa mbinu zinazoweza kusaidia kuongeza wanachama, kwa
kuwa unatoa nafasi ya kukutana nao ana kwa ana na kuwapa elimu kuhusu taratibu
za uanachama.
Maduka pia alisisitiza umuhimu wa wanachama kulipa ada kwa
wakati ili kutimiza wajibu wao na kuendelea kuwa wanachama hai, akiwataka
viongozi wa Jumuiya ya Wazazi katika ngazi za kata kuweka kipaumbele katika
zoezi la uandikishaji.
Alieleza kuwa mbinu za kutembelea watu duka kwa duka, nyumba
kwa nyumba na maeneo mengine zinaweza kusaidia kuwafikia wananchi ambao
hawajapata fursa ya kujiandikisha au kupata kadi za uanachama.
Aidha, aliwataka viongozi wa jumuiya kushirikiana na maafisa
wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa CCM Wilaya ya Mpanda
kurahisisha usajili wa wanachama kupitia mifumo ya kielektroniki, pamoja na
kuimarisha ufuatiliaji wa malipo ya ada.
Kwa upande wao, wafanyabiashara waliofikiwa na zoezi hilo
wameeleza kufurahishwa na utaratibu wa kutembelewa katika maeneo yao ya
biashara, wakisisitiza umuhimu wa kuendelea kutolewa kwa elimu kuhusu uanachama
wa CCM na jumuiya zake.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akimkabidhi Ndg. Dkt. Ruth Nakese Twange kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi, Oktoba 28, 2026. Zoezi hilo ni sehemu ya mwendelezo wa juhudi za kutafuta na kuandikisha wanachama wapya kupitia utaratibu wa kutembelea nyumba kwa nyumba. Ndg. Dkt. Ruth ameahidi kudumisha umoja na mshikamano katika kuijenga Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akimkabidhi Ndg. Self Ibrahim Ntija kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania, tarehe 28 Oktoba 2026, baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi. Ndg. Self ameahidi kudumisha umoja na mshikamano katika kuijenga jumuiya hiyo, kuitumikia CCM na Jumuiya ya Wazazi kwa moyo wa kujitolea, kulipa ada ya uanachama kwa mujibu wa taratibu, pamoja na kuhamasisha wengine kujiunga na jumuiya hiyo.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akimkabidhi Ndg. Rogers Andrew Marandu kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi. Ndg. Rogers ameahidi kudumisha umoja na mshikamano katika kuijenga jumuiya hiyo, pamoja na kulipa ada ya uanachama kikamilifu kwa mujibu wa taratibu.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akimkabidhi Ndg. Juma Omary Ngasa kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania, tarehe 28 Oktoba 2026, baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi. Ndg. Juma ameahidi kuwa mwanachama mwaminifu kwa kutimiza wajibu wake wa kulipa ada ya uanachama kwa mujibu wa taratibu.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akimkabidhi Ndg. Flavia Ludovick Kaswalala kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi, Oktoba 28, 2026.
Ndg. Flavia amefurahi na kushukuru kwa kupokea kadi hiyo, huku akiahidi kudumisha umoja na mshikamano katika kuijenga Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda. Pia, amesisitiza umuhimu wa kulipa ada ya uanachama kwa wakati ili kuendelea kuwa mwanachama hai, akihimiza kuendelezwa kwa zoezi la uandikishaji wa wanachama wapya kwa kutembelea wafanyabiashara duka kwa duka.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akimkabidhi Ndg. Filbeth Lucian Masawe kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi. Ndg. Filbeth ameeleza furaha na shukrani zake kwa kupokea kadi hiyo, huku akiahidi kudumisha umoja na mshikamano katika kuijenga Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, kuhamasisha wengine kujiandikisha na kukamilisha taratibu za uanachama, pamoja na kulipa ada ya uanachama kikamilifu kwa mujibu wa taratibu.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, akimkabidhi Ndg. Edina Amani Saidi kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi, Oktoba 28, 2026. Ndg. Edina ameahidi kudumisha umoja na mshikamano katika kuijenga Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, kulipa ada ya uanachama kwa mujibu wa taratibu, pamoja na kuhamasisha wengine kujiandikisha na kukamilisha taratibu za uanachama wa CCM kupitia Jumuiya ya Wazazi.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akimkabidhi Ndg. Plackzeda Costantino Makombe kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania, tarehe 28 Oktoba 2026, baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi. Ndg. Plackzeda ameahidi kudumisha umoja na mshikamano katika kuijenga jumuiya hiyo, pamoja na kulipa ada ya uanachama kwa wakati ili kuendelea kuwa mwanachama hai.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akimkabidhi Ndg. Catherine Gasper Isumba kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania, tarehe 28 Oktoba 2026, baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi. Ndg. Catherine ameeleza furaha na shukrani zake kwa kupokea kadi hiyo, huku akiahidi kulipa ada ya uanachama kikamilifu kwa mujibu wa taratibu.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akimkabidhi Ndg. Nelson Emmanuel Ndegeulaya, mkazi wa Kata ya Misunkumilo, kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania, tarehe 28 Oktoba 2026, baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi. Ndg. Nelson ameahidi kuwa mwaminifu katika kulipa ada ya uanachama kwa mujibu wa taratibu, pamoja na kuhamasisha wengine kujiunga na Jumuiya ya Wazazi.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akimpatia elimu ya uanachama Ndg. Marco Raphael Kandege na kumkabidhi kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania, tarehe 28 Oktoba 2026, baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi. Ndg. Marco ameahidi kuwa mwanachama mwaminifu kwa kulipa ada ya uanachama wake kwa mujibu wa taratibu.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akimkabidhi Ndg. Issa Juma Salumu kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi. Ndg. Issa amefurahi na kushukuru kwa kupata kadi hiyo, akieleza kuwa hatua hiyo imetokana na mapenzi yake kwa CCM. Ameahidi kudumisha umoja na mshikamano katika kuijenga Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, pamoja na kulipa ada ya uanachama kikamilifu na kwa wakati kwa mujibu wa taratibu za jumuiya.PROFESSOR MGOKO EPISODE 07
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment