Mwenyekiti wa Red Cross Mkoa wa Shinyanga na mjumbe wa Bodi Taifa Hatibu Mgeja leo tarehe 25.10.2026 amezindua Tawi jipya la Red Cross KIDANDA kata ya Itwangi, Wilaya ya ShinyangaAkizungumza wakati wa uzinduzi huo Mwenyekiti Mgeja aliwapongeza wanachama na voluntia kwa kujiunga kwenye chama hicho cha kibinadamu. "Mmefanya maamuzi sahihi na ya kimungu. Red Cross ni taasisi isiyofungamana na imani na itikadi yoyote. Hivyo niwaombe muongozwe na moyo wa huruma na upendo wakati wa kuihudumia jamii yetu".Katika uzinduzi huo, Mwenyekiti Mgeja alikata keki ikiwa ni ishara ya upendo na umoja kwa wanachama wote. Katika hatua nyingine Mgeja aliwahamisha wanachama hao kuanzisha mfuko wa hisa ili kujijengea uwezo na kupunguza utegemezi wa ufadhiri kutoka nje. Aidha, Mgeja aliwahamisha jitafuta eneo au kiwanja ili kujengwa kwa ofisi ya Red Cross tawi la KIDANDA na kuahidi kuchangia katika ujenzi huo. Sambamba, Mgeja alikuwakumbusha wanachama na wananchi kuhusu uwepo wa mvua hatari za El Nino na kuwasihi kuchukua tahadhari. Akijibu Risala ya tawi hili, Mgeja aliahidi kunzisha ligi ya mkoa wa Red Cross ya mpira wa miguu ili kuweza kuwakutanisha vijana wa taasisi hiyo pamoja kukuza vipaji. Mwisho, Mgeja aliuongeza uongozi wa Kijiji cha KIDANDA na Kata ya Itwangi kwa kushirikiana vizuri na Red Cross Mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa Red Cross Mkoa wa Shinyanga na mjumbe wa Bodi Taifa Hatibu Mgeja akizungumza.

PROFESSOR MGOKO EPISODE 07
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

















































































































































Post a Comment