" KATIBU WA CCM WILAYA YA MPANDA AFANYA KIKAO MAALUMU CHA HALMASHAURI KUU YA CCM WILAYA

KATIBU WA CCM WILAYA YA MPANDA AFANYA KIKAO MAALUMU CHA HALMASHAURI KUU YA CCM WILAYA

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mpanda, Mussa Ramadhani Mwevi, amefanya kikao maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya hiyo kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa majukumu ya chama, hali ya uhai wa chama katika ngazi mbalimbali za uongozi pamoja na kubaini maeneo yanayohitaji maboresho katika uendeshaji wa shughuli za chama.

Kikao hicho kilichofanyika Oktoba 25, 2026, ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya CCM kwa mujibu wa kalenda ya vikao elekezi ya chama kwa mwaka 2026, ambapo wajumbe walipata fursa ya kupitia hali ya chama wilayani humo na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uongozi, mahusiano na wananchi, uchumi wa chama, maadili pamoja na matumizi ya teknolojia katika shughuli za kila siku.

Katika tathmini ya uhai wa chama na mahusiano na wananchi, kikao kilibaini kuwa shughuli za chama katika ngazi za shina, tawi, kata na wilaya zinaendelea kutekelezwa, huku vikao vikiendeshwa kwa kuzingatia kalenda ya vikao vya CCM ya mwaka 2026 pamoja na utekelezaji wa maamuzi yanayotolewa katika vikao husika.

Kwa mujibu wa tathmini hiyo, utekelezaji wa vikao na maamuzi yake ni sehemu ya utaratibu unaolenga kuimarisha usimamizi wa shughuli za chama katika ngazi mbalimbali za uongozi na kuhakikisha majukumu yaliyopangwa yanafanyika kwa wakati.

Hata hivyo, katika eneo la uchumi wa chama, kikao hicho kilibaini changamoto ya upatikanaji wa vyanzo vya mapato vya uhakika katika ngazi za shina, tawi na kata, hali inayohusishwa na ukosefu wa vitega uchumi vinavyoweza kusaidia kugharamia shughuli za chama.

Changamoto hiyo imeonesha umuhimu wa kutafuta na kuimarisha vyanzo endelevu vya mapato katika ngazi hizo ili kuongeza uwezo wa kifedha wa chama na kusaidia utekelezaji wa majukumu yake bila kutegemea vyanzo vichache vya mapato.

Katika eneo la maadili, uwajibikaji, itikadi na uongozi, kikao kilitathmini utekelezaji wa katiba, kanuni na miongozo ya chama, kikibainisha kuwa CCM Wilaya ya Mpanda inaendelea kuzingatia taratibu hizo katika kusimamia shughuli zake.

Aidha, kikao kilijadili namna chama kinavyosimamia nidhamu na uwajibikaji wa viongozi na watendaji wake, ikiwemo kuchukua hatua za kinidhamu pale inapobainika kuwa kuna ukiukwaji wa maelekezo na misingi ya maadili ya chama.

Katika kuimarisha uelewa wa viongozi na wanachama, CCM Wilaya ya Mpanda imeeleza kuwa inaendelea kutekeleza programu za mafunzo ya itikadi, uongozi na maadili kuanzia ngazi ya shina, tawi, kata hadi wilaya, kwa lengo la kuwajengea uwezo viongozi na wanachama katika kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia misingi ya chama.

Kuhusu masuala ya kiutawala na kiutumishi, tathmini ya kikao ilibainisha kuwa mahusiano kati ya viongozi waliochaguliwa na watumishi wa chama ni mazuri, huku malalamiko yanayowasilishwa na viongozi, watumishi na wanachama yakishughulikiwa kwa wakati na hatua za kinidhamu kuchukuliwa pale inapohitajika.

Katika eneo la ushindani wa kisiasa, upashanaji wa taarifa na matumizi ya teknolojia, kikao kilitathmini uwezo wa chama na watendaji wake kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) katika kurahisisha mawasiliano na kutekeleza majukumu ya chama.

Tathmini hiyo ilibainisha kuwa matumizi ya mifumo ya kidijitali yamechangia kurahisisha ukusanyaji, uhifadhi na usambazaji wa taarifa, pamoja na kuboresha mawasiliano ya ndani ya chama na yale yanayohusisha wananchi.

Vilevile, matumizi ya majukwaa ya kidijitali katika mawasiliano na wananchi yalitajwa kuwa sehemu ya juhudi za kuimarisha upashanaji wa taarifa, uwajibikaji wa viongozi na mawasiliano ya chama kwa umma.

Pamoja na hatua hizo, kikao kilibaini kuwa bado kuna umuhimu wa kuboresha zaidi upatikanaji wa vifaa vya kisasa, mafunzo kwa watendaji na mifumo ya kiteknolojia, ikiwemo usalama wa taarifa, ili kukidhi mahitaji yanayotokana na mabadiliko ya teknolojia.

Kwa ujumla, kikao hicho maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Mpanda kimeweka msisitizo katika kuendelea kusimamia utekelezaji wa majukumu ya chama, kuimarisha uhai wake katika ngazi zote, kuboresha vyanzo vya mapato na kuongeza matumizi ya teknolojia katika shughuli za uongozi na mawasiliano.

Katibu wa CCM Wilaya ya Mpanda, Mussa Ramadhani Mwevi, akimwakilisha Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mpanda, Joseph Lwamba, akisalimia na kuwakaribisha wajumbe wa Kikao Maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Mpanda kilichofanyika Oktoba 25, 2026, katika Ukumbi wa CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi. Baada ya kuwakaribisha wajumbe, Mwevi alifungua rasmi kikao hicho kilicholenga kujadili na kuchangia mawazo kuhusu ajenda mbalimbali za chama.Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Mwa nisawa, akishiriki kikao Maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Mpanda kilichofanyika Oktoba 25, 2026, kwa lengo la kufanya tathmini ya hali ya chama wilayani humo na kupitia utekelezaji wa majukumu yake katika ngazi mbalimbali.Mjumbe wa Kamati ya Siasa na Kamati ya Maadili ya CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Kaswiza, akishiriki kikao Maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Mpanda kilichofanyika Oktoba 25, 2026, kwa lengo la kufanya tathmini ya hali ya chama wilayani humo na kupitia utekelezaji wa majukumu yake katika ngazi mbalimbali.Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, wakiwa katika Kikao Maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Mpanda kilichofanyika Oktoba 25, 2026, kwa lengo la kufanya tathmini ya hali ya chama na kupitia utekelezaji wa majukumu yake wilayani humo.Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akiwa katika Kikao Maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Mpanda kilichofanyika Oktoba 25, 2026, kwa ajili ya kufanya tathmini ya hali ya chama na kujadili utekelezaji wa majukumu yake wilayani humo.Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Wilaya ya Mpanda, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Sekretarieti ya CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, akishiriki Kikao Maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Mpanda kilichofanyika Oktoba 25, 2026, kwa lengo la kufanya tathmini ya hali ya chama na kupitia utekelezaji wa majukumu yake wilayani humo.Katibu wa CCM Wilaya ya Mpanda, Mussa Ramadhani Mwevi, akimwakilisha Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mpanda, Joseph Lwamba, akiongoza Kikao Maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, kilichofanyika Oktoba 25, 2026. Katika kikao hicho, Mwevi aliwapa nafasi wajumbe kuchangia mawazo, kutoa ushauri, maoni na nyongeza, pamoja na kuwasilisha shukrani na kujadili masuala mbalimbali yaliyohusu ajenda za kikao hicho.Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Mpanda, Irene, akishiriki kikao Maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Mpanda kilichofanyika Oktoba 25, 2026. Katika kikao hicho, Katibu wa CCM Wilaya ya Mpanda, Mussa Ramadhani Mwevi, alimkaribisha Irene kusoma ajenda zilizokuwa zimepangwa kujadiliwa, ili kuwawezesha wajumbe kupitia na kuchangia mawazo yao kuhusu kila ajenda.Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, wakishiriki kikao Maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Mpanda kilichofanyika Oktoba 25, 2026, kwa lengo la kufanya tathmini ya hali ya chama wilayani humo, kupitia utekelezaji wa majukumu yake na kujadili maeneo mbalimbali yanayohitaji kuimarishwa.Wajumbe wakiwa katika Kikao Maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, kilichofanyika Oktoba 25, 2026, kwa lengo la kufanya tathmini ya hali ya chama na kujadili utekelezaji wa majukumu yake wilayani humo.PROFESSOR MGOKO EPISODE 07

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





 

Post a Comment

Previous Post Next Post