" KATIBU WA JUMUIYA YA WAZAZI CCM MPANDA JIMOTOLI MADUKA AANDIKISHA WANACHAMA WAPYA 19 KWA KUTEMBELEA MADUKA

KATIBU WA JUMUIYA YA WAZAZI CCM MPANDA JIMOTOLI MADUKA AANDIKISHA WANACHAMA WAPYA 19 KWA KUTEMBELEA MADUKA

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mpanda, Jimotoli Jilala Maduka, ametembelea maduka ya wafanyabiashara katika Mji wa Mpanda, mkoani Katavi, kwa lengo la kuhamasisha uandikishaji wa wanachama wapya wa CCM na Jumuiya ya Wazazi.

Katika zoezi hilo lililofanyika Oktoba 27, 2026, jumla ya wanachama wapya 19 walijiandikisha kupitia CCM na Jumuiya ya Wazazi, huku wanachama tisa wakilipa ada zenye jumla ya Shilingi 27,600.

Akiwa katika ziara hiyo, Maduka alitumia fursa hiyo kuzungumza na wafanyabiashara kuhusu umuhimu wa kujiunga na chama na jumuiya zake, pamoja na kuhakikisha wanakamilisha taratibu za uanachama ili kuwa wanachama hai.

Pia, aliwahimiza wanachama kujisajili kwa wakati kupitia mifumo ya kielektroniki na kusisitiza umuhimu wa kulipa ada za uanachama kwa mujibu wa taratibu za chama.

Kwa mujibu wa maelezo ya zoezi hilo, wafanyabiashara walifurahishwa na utaratibu wa kutembelewa katika maeneo yao ya biashara, wakieleza kuwa njia hiyo inasaidia kuwafikia wanachama na wananchi wengi zaidi, hususan wale ambao hawana kadi za CCM au za jumuiya zake.

Maduka amesema mbinu ya kukutana na watu ana kwa ana, duka kwa duka na nyumba kwa nyumba ni miongoni mwa njia zinazoweza kusaidia kuongeza wanachama na kuimarisha uhai wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Wilaya ya Mpanda.

Zoezi hilo ni sehemu ya juhudi za kuhamasisha ushiriki wa wanachama katika shughuli za chama na jumuiya zake, zikiwemo Jumuiya ya Wazazi, Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akimkabidhi kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania Ndg. Shadrack Idrisa Haruna, baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama wa CCM kupitia Jumuiya ya Wazazi, Oktoba 27, 2026.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akimkabidhi Ndg. Peter Mhula kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi, Oktoba 27, 2026. Ndg. Peter amefurahi na kushukuru kwa kupokea kadi hiyo, huku akiahidi kuwa mwanachama mwaminifu kwa kulipa ada ya uanachama kwa wakati, kudumisha umoja na mshikamano, na kushiriki katika kuijenga Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post