" MSAMBARA YAPOKEA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 838 KWA AJILI YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA

MSAMBARA YAPOKEA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 838 KWA AJILI YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA

Wananchi wa Kata ya Msambara, Halmashauri ya Mji Kasulu, Mkoa wa Kigoma wamepokea kwa furaha taarifa ya Serikali kutoa zaidi ya shilingi milioni 838.612 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya katika kata hiyo, hatua inayolenga kuboresha huduma za afya na kupunguza changamoto za upatikanaji wa matibabu kwa wananchi wa Msambara na maeneo jirani.Furaha hiyo imejidhihirisha kupitia mwitikio wa wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika baada ya viongozi kutembelea eneo la mradi, ambapo  wananchi wameahidi kushirikiana na Serikali katika hatua zote za ujenzi ili kuhakikisha kituo hicho kinakamilika kwa wakati na kinakuwa na manufaa yaliyokusudiwa kwa jamii.Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Ayubu Ngalaba Kilugu, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wananchi na viongozi katika kusimamia na kutekeleza miradi ya maendeleo huku akiwataka wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali zinazolenga kuboresha maisha yao.Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Mwl. Vumilia Julius Simbeye, amewahimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za ujenzi na kuwa tayari kujiunga na kamati zitakazoundwa kwa ajili ya kusimamia mradi, kulinda vifaa na kuhakikisha miundombinu inayojengwa inatunzwa wakati wa utekelezaji na baada ya kukamilika.Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo, Nangi W. Nangi, ametoa wito kwa wananchi kutumia fursa ya Bima ya Afya kwa Wote ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za matibabu  akiwakumbusha kuzingatia kanuni za afya na usafi wa mazingira ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu pamoja na kujenga uelewa kuhusu kinga dhidi ya ugonjwa wa Ini.Wananchi wameishukuru Serikali kwa kutenga fedha hizo, wakieleza kuwa kukamilika kwa kituo hicho kutakuwa suluhisho muhimu kwa changamoto za huduma za afya, ikiwemo kupunguza umbali wa kufuata matibabu na kuboresha upatikanaji wa huduma kwao na wakazi wa maeneo jirani.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Mwl. Vumilia Julius Simbeye akizungumza.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post