" WANACHAMA WAPYA 8 WAANDIKISHWA, WALIPA ADA YA SHILINGI 19,200 KUPITIA ZOEZI LA DUKA KWA DUKA MPANDA

WANACHAMA WAPYA 8 WAANDIKISHWA, WALIPA ADA YA SHILINGI 19,200 KUPITIA ZOEZI LA DUKA KWA DUKA MPANDA

Zoezi la kuandikisha wanachama wapya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mpanda limeendelea kupamba moto baada ya wanachama wapya wanane kuandikishwa katika ziara ya kutembelea maduka ya wafanyabiashara mjini Mpanda, Oktoba 29, 2026.

Zoezi hilo limeongozwa na Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Jimotoli Jilala Maduka, ambaye ametembelea baadhi ya maduka kwa lengo la kuwasalimia wafanyabiashara, kutoa elimu ya uanachama na kusajili wanachama wapya.

Katika zoezi hilo, wanachama wapya wanane wamejiandikisha kupitia CCM na Jumuiya ya Wazazi, huku wote wakilipa ada ya uanachama yenye jumla ya Shilingi 19,200.

Maduka amesema kuwa utaratibu wa kuwafuata wanachama katika maeneo yao ya shughuli za kila siku, ikiwemo madukani na majumbani, ni muhimu katika kuwafikia watu wengi zaidi na kuongeza ushiriki wao katika chama na jumuiya zake.

Amesisitiza umuhimu wa kutoa elimu kuhusu taratibu za uanachama, upatikanaji wa kadi na ulipaji wa ada, akieleza kuwa hatua hizo zinasaidia wanachama kutambua wajibu wao na kudumisha uhai wa jumuiya.

Aidha, amewahimiza makatibu wa Jumuiya ya Wazazi katika ngazi za kata kuweka kipaumbele katika zoezi la uandikishaji kwa kutembelea maeneo mbalimbali, yakiwemo maduka, nyumba na maeneo mengine yenye uwezekano wa kuwafikia wanachama wapya.

Amesema kuwa juhudi hizo zinahitaji ushirikiano wa viongozi wa jumuiya na maafisa wa TEHAMA wa CCM Wilaya ya Mpanda ili kurahisisha usajili wa wanachama kwa njia ya kielektroniki na kuhakikisha taratibu za uanachama zinafuatwa.

Kwa upande wao, wafanyabiashara walioshiriki katika zoezi hilo wameeleza kufurahishwa na utaratibu wa kutembelewa katika maeneo yao ya kazi, wakisisitiza umuhimu wa kuendelea kutoa elimu ya uanachama na kuwafikia watu wengi zaidi.

Zoezi hilo ni mwendelezo wa juhudi za Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda katika kusajili wanachama wapya, kuhamasisha ulipaji wa ada na kuimarisha shughuli za jumuiya katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, akiendelea na zoezi la kuwafikia wanachama katika maeneo yao ya biashara kwa ajili ya kuwasalimia na kutoa elimu ya uanachama wa CCM na Jumuiya ya Wazazi, amemkabidhi Ndg. Neema Khalid Mohamed kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania, tarehe 29 Oktoba 2026, baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama wa CCM kupitia Jumuiya ya Wazazi. Ndg. Neema ameeleza furaha na shukrani zake kwa kupokea kadi hiyo, huku akiahidi kuwa mwaminifu katika kulipa ada ya uanachama wa CCM na Jumuiya ya Wazazi kwa mujibu wa taratibu.Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akiendelea kuwafikia wananchi, wakiwemo wapenzi wa soka, kwa ajili ya kutoa elimu ya uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi, amemkabidhi Ndg. Habibu Mengi kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania, tarehe 29 Oktoba 2026, baada ya kupata elimu na kujiandikisha kuwa mwanachama wa CCM kupitia jumuiya hiyo. Ndg. Habibu ameeleza shukrani zake kwa kupokea kadi hiyo, huku akiahidi kulipa ada ya uanachama kwa wakati na kwa mujibu wa taratibu.Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akimpatia elimu ya uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi Ndg. Saumu Justine Mlingi, kabla ya kumkabidhi kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama. Ndg. Saumu ameahidi kuwa mwaminifu katika kulipa ada ya uanachama kwa wakati na kwa mujibu wa taratibu.


Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akimkabidhi Ndg. Samson Elias Andrew maarufu kama Samswaga, kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania, tarehe 29 Oktoba 2026, baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi. Ndg. Samson ameeleza furaha na shukrani zake kwa kupokea kadi hiyo, huku akiahidi kudumisha umoja na mshikamano katika kuijenga jumuiya hiyo, kushirikiana na wanachama wengine kuendeleza shughuli zake, pamoja na kuwa mwaminifu katika kulipa ada ya uanachama wa CCM na Jumuiya ya Wazazi.

PROFESSOR MGOKO EPISODE 07

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment

Previous Post Next Post