Wakazi wa
Mtaa wa Mbuyuni Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga wamejitokeza kufanya
usafi wa mazingira ikiwa ni maandalizi ya kujikinga na madhara yanayoweza
kujitokeza kutokana na mvua za El Nino zinazotarajiwa kunyesha hivi karibuni.
Zoezi hilo
limehusisha usafishaji wa mitaro, kuondoa taka ngumu na kufyeka vichaka katika
barabara kuu inayoelekea Mtaa wa Dome, ambayo imetajwa kuwa ni miongoni mwa
maeneo korofi yanayokumbwa na mafuriko mara kwa mara.
Akizungumza
wakati wa zoezi hilo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbuyuni, Bwana Seif Nassor Mohamed
amesema zoezi hilo ni endelevu na linalenga kuhakikisha mtaa unabaki kuwa safi
na salama.
Aidha,
Mwenyekiti huyo amewataka wananchi kuchukua tahadhari mapema kutokana na dalili
za mvua hizo kuonekana tayari katika baadhi ya maeneo ya mtaa huo.
Kwa upande
wake, Mkazi wa Mtaa huo, Bwana Shaban ambaye alishiriki vema katika zoezi hilo,
amewahimiza wananchi wenzake kuwa na umoja na mshikamano katika kuhakikisha
mtaa wao unakuwa safi na salama wakati wote, siyo tu wakati wa mvua.
Naye Bi.
Khadija Masenza, mkazi wa Mbuyuni, amesema usafi wa mitaro ni kipaumbele kwao
kutokana na historia ya mtaa huo kujaa maji.
Zoezi la
usafi wa mazingira katika Mtaa wa Mbuyuni linatajwa kuwa ni mfano wa kuigwa,
ambapo wananchi wenyewe ndio wamekuwa mstari wa mbele bila kusubiri Manispaa,
ikiwa ni utekelezaji wa kauli mbiu isemayo "Usafi ni Afya".


PROFESSOR MGOKO EPISODE 07
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254







Post a Comment