
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema uamuzi wa kizalendo uliofanywa na Serikali umewezesha kukamilika kwa Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere (JNHPP), uliokuwa sehemu ya ndoto kubwa ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Dkt. Mwigulu ameyasema hayo leo Novemba 8, 2026 wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero zao uliofanyika Wilaya ya Kishapu, Mkoa wa Shinyanga.
Dkt. Mwigulu ameeleza kuwa utekelezaji wa Ilani za Uchaguzi za awamu tatu tofauti umechangia kwa kiasi kikubwa kupanua upatikanaji wa umeme nchini, ambapo awali Serikali ililenga kufikisha umeme katika makao makuu ya wilaya, baadaye katika kata na hatimaye vijiji vyote nchini.
Ameongeza kuwa kwa sasa Serikali inaendelea kupanua huduma ya umeme hadi katika vitongoji, maeneo ya migodi midogo na mikubwa pamoja na viwanda ili kuongeza fursa za kiuchumi na kuchochea maendeleo ya wananchi.
Akizungumzia kukamilika kwa Mradi wa JNHPP, Dkt. Mwigulu amesema Serikali ilikabiliwa na maamuzi mawili muhimu, ambayo ni kukodi mitambo ya kuzalisha umeme au kuelekeza nguvu katika kukamilisha ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere.
Amesema Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, iliamua kwa uzalendo kukamilisha mradi huo badala ya kutumia fedha kukodi mitambo ambayo isingekuwa mali ya Serikali.
Amefafanua kuwa uamuzi huo umewezesha kukamilika kwa bwawa hilo, huku shughuli za uzalishaji umeme zikiendelea, na hivyo kutimiza ndoto ya muda mrefu ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere ya kuwa na mradi mkubwa wa kuzalisha umeme kwa kutumia rasilimali za maji nchini.

PROFESSOR MGOKO EPISODE 07
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment