Katibu wa
Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, ameendelea
na zoezi la uandikishaji wa wanachama wapya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na
Jumuiya ya Wazazi kwa kutembelea wafanyabiashara katika maduka yao pamoja na
maeneo ya wamachinga na mamalishe mjini Mpanda.
Katika zoezi
hilo lililofanyika Novemba 7, 2026, Katibu huyo alitembelea baadhi ya maduka
katika Kata ya Majengo, akizungumza na wafanyabiashara, kutoa elimu ya
uanachama na kuwaandikisha wale walioamua kujiunga na CCM pamoja na Jumuiya ya
Wazazi.
Jumla ya
wanachama wapya 25 waliandikishwa katika zoezi hilo na kukabidhiwa kadi za
Umoja wa Wazazi wa Tanzania baada ya kukamilisha taratibu za uanachama.
Akizungumza
na wafanyabiashara hao, Jimotoli aliwahimiza wanachama na viongozi wa jumuiya
kuendelea kuhamasisha watu kujiunga na chama na jumuiya zake, ikiwemo Jumuiya
ya Wazazi, Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).
Alieleza
kuwa njia ya kukutana na watu ana kwa ana kwa kutembelea maduka, nyumba kwa
nyumba na maeneo mbalimbali ni miongoni mwa mbinu zinazoweza kuwafikia watu
wengi zaidi, wakiwemo wale ambao bado hawajajiandikisha au hawana kadi za
uanachama.
Aidha,
alisisitiza umuhimu wa wanachama kutambua wajibu wa kulipa ada kwa mujibu wa
taratibu za chama na jumuiya ili kudumisha uhai wa uanachama wao.
Jimotoli pia
amewataka makatibu wa Jumuiya ya Wazazi katika ngazi ya kata kulipa kipaumbele
zoezi la uandikishaji kwa kuwafikia wananchi katika maeneo yao, akisisitiza
kuwa jukumu hilo linahitaji ushirikiano wa viongozi pamoja na maafisa TEHAMA wa
CCM Wilaya ya Mpanda ili kurahisisha usajili kwa njia ya kielektroniki.
Kwa upande
wao, baadhi ya wafanyabiashara waliofikiwa katika zoezi hilo wameeleza
kufurahishwa na utaratibu wa viongozi kuwafuata katika maeneo yao ya shughuli
za kiuchumi, wakisema unawapa fursa ya kupata elimu ya uanachama na kushiriki
katika mchakato wa kujiandikisha.
Zoezi hilo ni sehemu ya juhudi za Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda katika kuhamasisha uandikishaji wa wanachama wapya, kuimarisha uhai wa jumuiya na kuongeza ushiriki wa wanachama katika shughuli zake.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akiendelea na zoezi la kutembelea mama lishe katika Kata ya Majengo, kuwasalimia na kuwapatia elimu ya uanachama wa Chama Cha Mapinduzi. Katika zoezi hilo lililofanyika Novemba 7, 2026, alimkabidhi Ndg. Maria Jumanne Makala kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama mpya. Kwa upande wake, Maria ameshukuru kwa kutembelewa na kupewa elimu ya uanachama, huku akiahidi kutimiza wajibu wake wa kulipa ada ya uanachama kwa mujibu wa taratibu.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akimkabidhi Ndg. Ally Rashid Mayaya kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania, Novemba 7, 2026, baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama mpya wa Chama Cha Mapinduzi kupitia Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda. Ally ameshukuru kwa viongozi kuendelea kuwafikia katika maeneo yao ya kazi na kuwapatia elimu ya uanachama, huku akiahidi kutimiza wajibu wake wa kulipa ada ya uanachama kwa mujibu wa taratibu.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akimkabidhi Ndg. Gervas Diamond Chibula kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania baada ya kumtembelea dukani kwake, kumsalimia na kumpatia elimu ya uanachama wa Chama Cha Mapinduzi. Ndg. Gervas alijiandikisha kuwa mwanachama mpya kupitia Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda na kuahidi kuwa mwaminifu katika kulipa ada ya uanachama kwa mujibu wa taratibu.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Novemba 7, 2026, akimkabidhi Ndg. Musa Gibogo Mchuma kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania baada ya kumtembelea, kumsalimia na kumpatia elimu ya uanachama wa Chama Cha Mapinduzi. Baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama mpya kupitia Jumuiya hiyo, Ndg. Musa ameahidi kudumisha umoja na mshikamano katika kuijenga Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda pamoja na kutimiza wajibu wake wa kulipa ada ya uanachama kwa mujibu wa taratibu.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Novemba 7, 2026, akiendelea kuwafikia mafundi wa baiskeli katika Wilaya ya Mpanda kwa ajili ya kutoa elimu ya uanachama na kuandikisha wanachama wapya. Katika zoezi hilo, alimkabidhi Ndg. Deus Thomas Siwezi kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama mpya kupitia Jumuiya hiyo, huku akiahidi kuwa mwaminifu katika kulipa ada ya uanachama kwa mujibu wa taratibu.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Novemba 7, 2026, akimkabidhi Ndg. Thomas Siwezi, fundi wa baiskeli, kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania baada ya kumtembelea na kumpatia elimu ya uanachama wa Chama Cha Mapinduzi. Ndg. Thomas alijiandikisha kuwa mwanachama mpya kupitia Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda na kuahidi kuwa mwaminifu katika kulipa ada ya uanachama kwa mujibu wa taratibu.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akiendelea na zoezi la kutafuta na kuandikisha wanachama wapya kwa kutembelea wafanyabiashara duka kwa duka katika Kata ya Majengo. Katika zoezi hilo, Ndg. Nicholaus Lameck Rubitse akikabidhiwa kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama mpya kupitia Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, huku akiahidi kuwa mwaminifu katika ulipaji wa ada ya uanachama kwa mujibu wa taratibu.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Novemba 7, 2026, akimkabidhi Ndg. Zubery Amiry Kasomba kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania baada ya kumpatia elimu ya uanachama na kujiandikisha kuwa mwanachama mpya wa Chama Cha Mapinduzi kupitia Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, huku akiahidi kuwa mwaminifu katika kulipa ada ya uanachama kwa mujibu wa taratibu.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Novemba 7, 2026, akimkabidhi Ndg. Ramadhan Risasi Mfaume kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania baada ya kumtembelea katika eneo lake la kazi na kumpatia elimu ya uanachama wa Chama Cha Mapinduzi. Baada ya kuelewa taratibu za uanachama, Ramadhan alijiandikisha kuwa mwanachama mpya kupitia Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, huku akishukuru kwa kufikiwa kazini kwake na kuahidi kutimiza wajibu wa kulipa ada ya uanachama.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Novemba 7, 2026, akimtembelea Ndg. Javis Lucas Kasegezya, fundi, katika eneo lake la kazi na kumpatia elimu ya uanachama wa Chama Cha Mapinduzi kupitia Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda. Baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama mpya, Javis alikabidhiwa kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania, huku akishukuru kwa viongozi kuwafikia mafundi na makundi mbalimbali katika maeneo yao ya kazi, akieleza kuwa hatua hiyo ni faraja kwake na kuahidi kuwa mwaminifu katika kulipa ada ya uanachama.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Novemba 7, 2026, akimtembelea Ndg. Festo Efrem Nastazio dukani kwake kwa ajili ya kumsalimia na kumpatia elimu ya uanachama wa Chama Cha Mapinduzi kupitia Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda. Baada ya kupata elimu hiyo, Festo aliridhia kujiandikisha kuwa mwanachama mpya na kuahidi kuwa mwaminifu katika kulipa ada ya uanachama wake kwa mujibu wa taratibu.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Novemba 7, 2026, akimtembelea Ndg. Adamu Omari, fundi cherehani, katika eneo lake la kazi kwa ajili ya kumsalimia na kumpatia elimu ya uanachama wa Chama Cha Mapinduzi kupitia Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda. Baada ya kupata elimu hiyo, Adamu alishukuru kwa kufikiwa na kujiandikisha kuwa mwanachama mpya, kisha akakabidhiwa kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Novemba 7, 2026, akimpatia Ndg. Revocatus Jacob Nondo elimu ya uanachama wa Chama Cha Mapinduzi kupitia Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, huku akiahidi kuwa mwaminifu katika kulipa ada ya uanachama wake kwa mujibu wa taratibu.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Novemba 7, 2026, akimtembelea Ndg. Ester Elias Zumbi, mama lishe, katika eneo lake la kazi kwa ajili ya kumsalimia na kumpatia elimu ya uanachama wa Chama Cha Mapinduzi kupitia Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda. Baada ya kupata elimu hiyo, Ester alishukuru na kukabidhiwa kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama mpya, huku akiahidi kulipa ada ya uanachama kwa wakati.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Novemba 7, 2026, akimtembelea Ndg. Ibrahim Salum Mnyawi katika eneo lake la kazi kwa ajili ya kumsalimia na kumpatia elimu ya uanachama wa Chama Cha Mapinduzi kupitia Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda. Katika ziara hiyo, Ibrahim alikabidhiwa kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama mpya, huku akishukuru kwa kufikiwa katika eneo lake la kazi na kuahidi kuwa mwaminifu katika kulipa ada ya uanachama kwa mujibu wa taratibu.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Novemba 7, 2026, akimtembelea Ndg. Mengi William katika eneo lake la kazi kwa ajili ya kumsalimia na kumpatia elimu ya uanachama wa Chama Cha Mapinduzi kupitia Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda. Baada ya kupata elimu hiyo, Mengi alijiandikisha kuwa mwanachama mpya na kukabidhiwa kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania, huku akiahidi kuwa mwaminifu katika kulipa ada ya uanachama kwa mujibu wa taratibu.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akiendelea kuwatembelea wafanyabiashara katika maeneo yao ya kazi kwa ajili ya kuwasalimia na kuwapatia elimu ya uanachama wa Chama Cha Mapinduzi. Katika zoezi hilo, Ndg. John Francis Mollel akikabidhiwa kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama mpya kupitia Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, huku akishukuru kwa kufikiwa katika eneo lake la kazi na kuahidi kuwa mwaminifu katika kulipa ada ya uanachama kwa mujibu wa taratibu.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Novemba 7, 2026, akimkabidhi Ndg. Khalifan Hamis kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania mara baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi kupitia Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, huku akiahidi kulipa ada ya uanachama wake kwa uaminifu.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akimkabidhi Ndg. Maulid Juma Abed kadi ya Umoja wa Wazazi wa Tanzania mara baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi kupitia Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, huku akiahidi kulipa ada ya uanachama kwa uaminifu.PROFESSOR MGOKO EPISODE 07
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254







Post a Comment