Abiria wa masafa marefu wamepatiwa elimu ya usalama barabarani kuhusu kukemea na kutoa taarifa pindi waonapo vitendo hatarishi vikifanywa na madereva wawapo safarini nyakati za usiku.Elimu hiyo imetolewa na Mkuu wa Kikosi Cha usalama barabarani Wilaya ya Shinyanga Mrakibu msaidizi wa Polisi Zainabu Mangara katika Stendi kuu ya Mabasi Mkoa wa Shinyanga ambapo amewataka abiria hao kupaza sauti zao Kwa kukemea vitendo ambavyo ni kinyume Cha Sheria ya usalama barabarani vikifanywa na madereva kama mwendokasi, kuyapita Magari mengine katika mazingira hatarishi, kuzidisha abiria au Kuendesha gari likiwa katika hali ya ubovu.Mrakibu wa Polisi Zainabu Mangara amewaeleza abiria hao kuwa kila mmoja anatakiwa kuwa balozi wa usalama barabarani Kwa kutii Sheria bila shuruti ili kujiepusha na ajali za barabarani hasa nyakati za usiku.Kwa upande wao abiria hao wamelipongeza Jeshi la Polisi Kwa kuendelea kuwafikia na kutoa elimu ya usalama barabarani nyakati zote kwani hatua hiyo inazidi kuwapa uelewa na kuchukua hatua kabla ya madhala kutokea.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 07
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment