" AKUTWA AMEJINYONGA HADI KUFA MLANGONI KIJIJI CHA SHILABELA MKOANI SHINYANGA

AKUTWA AMEJINYONGA HADI KUFA MLANGONI KIJIJI CHA SHILABELA MKOANI SHINYANGA

  


Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mzee mmoja anayefahamika kwa jina la Lugelesha Kusena Mwenye umri wa miaka 70 mkazi wa kijiji cha Shilabela kata ya Pandagichiza Halmashauri ya Shinyanga, amekutwa akiwa amejinyonga hadi kufa ndani ya Nyumba wanayoishi.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Ijumaa Novemba 4 Mwaka huu 2022 ambapo mzee Lugelesha Kusena alikutwa akiwa amejinyonga hadi kufa ndani ya Nyumba wanayoishi mlangoni kwa kutumia shuka lenye rangi nyeusi.

Taarifa hizo zimetolewa na  Mwenyekiti wa kijiji cha Shilabela  Emmanuel Magadula ambapo ameeleza namna alivyopokea taarifa za tukio hilo.

“Nilikutwa na vijana wawili ambao walitumwa na wasalama nikaondoka Nyumbani nilipofika kwenye tukio nikamkuta yule marehemu akiwa amejinyonga kwa kutumia nguo yeusi niliwapigia polisi baada ya kuja wakafanya uchunguzi wao ikabainika kwamba huyo marehemu alijinyonga sehemu mbili sasa tukashindwa kuelewa kwamba huyu marehemu alijinyonga kweli au hicho kifo kimesababishwa na watu wengine”.amesema Mwenyekiti wa kijiji Magadula

Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa kitongoji cha Bukoloji alipokuwa akiishi marehemu katika kijiji cha Pandagichiza Martin Bimo naye amekili kuumizwa na kifo cha mzee huyo huku akisema mazishi tayari yamefanyika leo Siku ya Jumamosi kwenye kitongoji hicho.

Misalaba Blog pamoja na kufanya jitihada mbalimbali za kumpata kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga bado haikufanikiwa kumpata.

Post a Comment

Previous Post Next Post