ASKOFU SANGU AENDELEA KUSHUHUDIA MOYO WA IMANI NA MAJITOLEO YA WAAMINI KWA KANISA, AIMARISHA WAKRISTO WAPYA 1,252
Misalaba0
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, ameendelea kushuhudia matunda ya moyo wa imani na majitoleo kwa Kanisa kutoka kwa Waamini, kupitia ziara ya kichungaji aliyoifanya hivi karibuni katika Parokia tatu za Mwamapalala Wilayani Itilima mkoani Simiyu, Mwandoya wilayani Meatu mkoani Simiyu na Maganzo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
Kupitia ziara hiyo, Askofu Sangu ametoa Sakramenti ya Kipaimara kwa idadi kubwa ya Wakristo wapya, wakubwa kwa wadogo, inayofikia watu 1,252, ambapo kati ya hao, 660 ni wa Parokia moja ya Mwamapalala , 450 ni wa Parokia ya Mwandoya na 142, ni wa Parokia ya Maganzo.
Pia, amebariki na kuzindua makanisa mapya mawili pamoja na Groto kwa ajili ya heshima kwa Mama Bikra Maria, kwenye vigango vya Ngh’omango na Mwalushu vilivyopo katika Parokia ya Mwamapalala, vilivyojengwa kwa nguvu za waamini kwa kushirikiana na wasamaria wema.
Halikadhalika, amefungua ukumbi mpya pamoja na kuweka jiwe la msingi katika jengo la utawala na maabara ya kisasa linaloendelea kujengwa katika shule ya Sekondari Mwamapalala, inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga.
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga, pamoja na kuwapongeza Waamini kwa namna ambavyo wametambua umuhimu wa kujitoa kwa ajili ya ustawi wa Kanisa lao, ameendelea kuwasisitiza kuwa na moyo wa imani na majitoleo kwa Kanisa , ambalo kwa sasa halitegemei tena misaada kutoka nje ya nchi kama ilivyokuwa hapo awali, na badala yake kazi ya umisionari imeachwa mikononi mwa Waafrika wenyewe.
Askofu Sangu pia ametumia nafasi hiyo kupeleka ujumbe wa amani na upendo kwa watu wote, huku akiwataka Wakristo kuwa na hofu ya Mungu kwa mambo yote wanayoyafanya, hali ambayo ameitaja kuwa itawawezesha kuepuka kushiriki katika matendo maovu yanayomchukiza mwenyezi Mungu, ambayo ni pamoja na kuziona shida za wengine kama fursa ya kujipatia kipato badala ya kuwasaidia, na kuwa chanzo cha chuki na mafarakano miongoni mwa jamii.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PAROKIA YA MWAMAPALALA
Mapokezi ya Askofu Sangu katika Parokia ya MwamapalalaAskofu Sangu akisalimiana na baadhi ya Waamini wa Parokia ya Mwamapalala mara baada ya kuwasili katika Parokia hiyoAskofu Sangu akizindua Kanisa la Kristo Mfalme Kigango cha Ngh’omangoAskofu Sangu akifungua Groto ya Mama Bikra Maria katika Kigango cha Ngh’omangoAskofu Sangu akitoa heshima kwa Mama Bikra Maria baada ya kufungua GrotoMuonekano wa nje wa Kanisa la Kristo Mfalme Kigango cha Ngh’omangoAskofu Sangu akiwa ndani ya Kanisala Kristo Mfalme baada ya kulifungua rasmiKanisa jipya la Kigango cha MwalushuMuonekano wa ndani wa Kanisa la Kigango cha MwalushuAskofu Sangu akiongoza sala kwa heshima ya Mama Bikra Maria mara baada ya kuzindua Kanisa na Groto katika Kigango cha MwalushuAskofu Sangu akipokelewa na wanafunzi katika shule ya Sekondari MwamapalalaAskofu Sangu akikata utepe kuzindua ukumbi wa shuleAskofu Sangu akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa jengo la utawala na maabara ya kisasa katika shule ya Sekondari MwamapalalaAskofu Sangu akisaini kitabu cha wageni katika shule ya Sekondari Mwamapalala, kulia ni mkuu wa shule hiyo Padre Joseph Komanya na wa pili kushoto ni Paroko wa Parokia ya Mwamapalala Padre Beatus MaduhuAskofu Sangu akiagana na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Mwamapalala mara baada ya kutembelea shule hiyo kama sehemu ya ziara yake katika Parokia ya MwamapalalaAskofu Sangu akiongoza Misa takatifu ya Kipaimara katika siku ya pili ya ziara yake katika Parokia ya MwamapalalaAskofu Sangu akitoa Sakramenti ya Kipaimara katika Parokia ya MwamapalalaAskofu Sangu akiendelea na adhimisho la Misa takatifu katika Parokia ya Mwamapalala, aliyeshika Mic ni Paroko msaidizi wa Parokia hiyo na mkuu wa shule ya Sekondari Mwamapalala Padre Joseph Komanya, wa kwanza kushoto ni Padre Paslay Marwa kutoka jimbo la Musoma na wa pili kushoto ni Paroko wa Parokia hiyo padre Beatus MaduhuAskofu Sangu akiwakomunisha waimarishwa katika Parokia ya MwampalalaBaadhi ya waamini wa Parokia ya Mwamapalala ikiwemo waimarishwa wakiwa katika adhimisho la Misa takatifu ya KipaimaraWanakwaya wa Parokia ya Mwamapalala na utoto mtakatifu wa Yesu wakiwa katika adhimisho la Misa takatifuWaimarishwa na waamini wakimtolea Mungu shukraniAskofu Sangu akikabidhi cheti cha pongezi kwa baadhi ya wanandoa ambao wamedumu kwa zaidi ya miaka 25
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PAROKIA YA MWANDOYA
Fratel Boniphace Seleka kutoka Parokia teule ya Lagangabilili akisoma somo la pili katika Misa ya Kipaimara iliyofanyika katika Parokia ya MwandoyaPadre Prasad George (SMA) akisoma somo la InjiliAskofu Sangu akitoa Homilia kwenye Misa ya Kipaimara katika Parokia ya MwandoyaAskofu Sangu kwa kushirikiana na Mapadre wa Parokia ya Mwandoya akiongoza sala maalum ya kwa ajili ya kuwaimarisha WaimarishwaAskofu Sangu akitoa Sakramenti ya Kipaimara katika Parokia ya MwandoyaMakatekista wa Parokia ya Mwandoya wakiwa kwenye Misa ya KipaimaraAskofu Sangu kwa kushirikiana na Mapadre wa Parokia ya Mwandoya akiendelea na adhimisho la Misa takatifuParoko msaidizi wa Parokia ya Mwandoaya Padre Michael Mick (SMA) akimkomnisha mmoja wa Waamini waliohudhuria MisaParoko wa Parokia ya Mwandoya Padre Marek Krysa (SMA) akiwakomunisha WaaminiPadre Prasad George (SMA) akiwakomunisha WaaminiAskofu Sangu akiwakomunisha WaimrishwaParoko wa Parokia ya Mwandoya Padre Marek Krysa (SMA)akitoa neno la shukrani kwa Mhashamu Baba AskofuUtoto mtakatifu wa Yesu Parokia ya Mwandoya katika picha ya pamoja na Mhashamu Baba Askofu SanguParoko msaidizi wa Parokia ya Mwandoaya Padre Michael Mick (SMA)akitoa neno la shukraniAskofu Sangu akizungumza na Waamini wa Parokia ya Mwandoya mara baada ya Misa na kuwashukuru kwa moyo wa imani na jitihada zao za kulitegemeza Kanisa
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PAROKIA YA MAGANZO
Mapokezi ya Askofu Sangu katika Kigango cha Idukilo Parokia ya MaganzoParoko wa Parokia ya Maganzo Padre Emmanuel Kahabi akimkaribisha Askofu Sangu katika kigango cha IdukiloAskofu Sangu akibariki na kuzindua Tabernakulo (chombo maalum cha kuhifadhia mwili na damu ya Kristo) katika Kigango cha IdukiloParoko wa parokia ya Maganzo Padre Emmanuel Kahabi akimkaribisha Mhashamu Baba Askofu kwa ajili ya adhimisho la Misa takatifu ya KipaimaraAskofu Sangu akitoa Homilia katika Misa ya KipaimaraKatibu wa Askofu Padre Deusdedith Kisumo akimkaribisha Paroko wa Parokia ya Maganzo kuwatambulisha Waimarishwa kwa AskofuParoko wa parokia ya Maganzo Padre Emmanuel Kahabi akiwatambulisha Waimarishwa kwa AskofuAskofu Sangu kwa kushirikiana na Mapadre akiongoza sala maalum ya kuwaimarisha WaimarishwaAskofu Sangu akitoa Sakramenti ya Kipaimara katika Parokia ya MaganzoAskofu Sangu akipokea matoleo katika Parokia ya MaganzoWaimarishwa wa Parokia ya Maganzo wakipeleka matoleo yaoWanakwaya wa Parokia ya Maganzo wakiwa katika MisaAskofu Sangu akiwakomunisha Waimarishwa katika Parokia ya MaganzoKatibu wa Askofu Padre Deusdedith Kisumo akiwakomunisha waaminiParoko wa parokia ya Maganzo Padre Emmanuel Kahabi akiwakomunisha wanakwayaAskofu Sangu akiwa na Paroko wa Parokia ya Maganzo Padre Emmanuel KahabiAskofu Sangu aktika Picha ya pamoja na makundi mbalimbali Parokiani MaganzoAskofu Sangu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Waimarishwa katika Parokia ya MaganzoParoko wa Parokia ya Maganzo Padre Emmanuel Kahabiakitoa neno la shukrani kwa AskofuBaadhi ya waamini wa Parokia ya Maganzo wakiwa kwenye eneo la MisaPicha ya pamoja na wawakilishi wa makundi mbalimbali ndani ya Kanisa
Post a Comment