Na Fabius Clavery Misalaba Blog,Kagera.
Mawakala wanaosajili laini za simu katika makampuni mbalimbali ya simu yaliyopo nchini wametakiwa kujiepusha na masuala ya udanganyifu wa kusajili laini za simu kwa kutumia namba za NIDA za watu wengine na kisha kuziuza kwa watumiaji wengine.
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU mkoani Kagera John Joseph wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu yake kwa robo ya mwaka ya julai hadi september kwa waandishi wa habari November 2 mwaka huu.
Akitoa taarifa hiyo bw,Joseph amesema kuwa mawakala watano wa usajili wa lainibza simu mkoani humo wanashilikiwa kufuatia kujihusisha na masuala uuzaji wa laini zenhe majina mengine kwa watu wengine.
"Tunawashikilia mawakala watano wa usajili wa laini za simu uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani,kutokana na ufuatiliaji ambao tumekuwa tukiufanya katika laini za simu za mkononi tumebaini kuna mawakala kutoka makampuni mbalimbali sio waaminifu na waadilifu wamekuwa wakiwasajilia baadhi ya watu laini kwa kutumia majina na vitambulisho vya watu wengine" ameeleza bwana Joseph.
Hata hivyo mkuu huyo wa TAKUKURU ametoa wito kwa wananachi kufatilia mara kwa mara taarifa za laini za simu ambazo zimesajiliwa kwa majina na namba za vitambulisho vyao (NIDA) kwani kuwepo kwa namba ambazo zimesajiliwa kwa vitambulisho vyao na hawazitambui zinaweza kutumiwa kufanya matukio ya uhalifu.
"Nitoe wito kwa wananchi kuwa na utaratibu wa kufika katika maduka ya watoa huduma mitandao yao ili kuhakiki namba zao na kama kuna ambazo hawazitumii wazifunge "aliongeza bw.Joseph Mkuu wa TAKUKURU Kagera.
Kadhalika TAKUKURU imebaini mapungufu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo 48 yenye thamani ya zaidi ya Bilion 16 ambayo ni ujenzi wa mradi wa vyumba vya madarasa, ujenzi wa mradi wa maegesho ya magari makubwa, mradi wa miundo mbinu ya maji, ujenzi wa vituo vya Afya na Zahanati pamoja na ujenzi wa vyoo.
mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU mkoani Kagera John Joseph
Post a Comment