" MASALIA YA VIFAA VYA KIVITA KUONDOLEWA MISSENYI MKOANI KAGERA

MASALIA YA VIFAA VYA KIVITA KUONDOLEWA MISSENYI MKOANI KAGERA

 



Na Fabius Clavery- Misalaba Blog, Kagera

Halmashauri ya wilaya ya misenyi mkoani Kagera inafanya jitihada za kukagua na kuondoa  masalia ya vifaa vya kivita katika kata ya Nsunga iliyopo wilayani humo kufuatia kulipotiwa kwa uwepo wa mabomu mara kwa mara katika kata hiyo ili kuwahakikishia usalama wakazi wa eneo hilo.

Hayo yalielezwa na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo kanali Willison Sakullo wakati akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani  cha halmashauri ya wilaya hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri mnamo october 28 mwaka huu .

Kanali Sakulo alikiambia kikao hicho kuwa tayari taratibu za kuwasiliana na wahusika kutoka vikosi vya jeshi zinaendelea kufanyika ambapo tayari halmashauri hiyo imekwisha andika barua kwenda kwa  mkuu wa mkoa wa Kageraili kuwezesha zoezi hilo.

"Ni kweli hili swala lilikwisha fika kwangu,na sisi kwa uzito wake tumeliandikia kwenda kwa mkuu wa mkoa ili liandikiwe kwenda makao makuu ya jeshi kuona kwamba wale wataalamu wanao husika na medani waje basi kufanya angalau upekuzi katika lile eneo maana naambiwa kuna maandaki pale yaliachachwa kipindi cha Idiamin vita ya Kagera,ni kama mara mbili tatu zimetokea taarifa limekutwa bomu sasa tusingependa wananachi wetu waendelee kudhulika" alisema Kanali Sakulo.

Kwa upande mwengine  mkuu huyo wa wilaya ametoa rai kwa madiwani kufuatilia ujenzi wa vyumba kumi vya madarasa vinavyojengwa katika kata za halmashauri hiyo ambazo ni kata za Kashenye, Buyango Bugandika Kilimilile Gabulanga Minziro Kakunyu na Kyaka ambapo vinajengwa vyumba viwili.

"mweshimiwa mwenyekiti nawaomba waheshimiwa madiwani wafuatilie pia katika huu ujenzi wa madarasa kumi yanayojengwa kama tulivyokuwa tunafanya kipindi kile cha fedha za uviko 19ili madarasa haya yamalizike mapema mimi wakati wa uzinduzi wangu kutokana na maelekezo ya mkuu wa mkoa nilitoa siku 35 ambazo zinaisha tarehe 25 mwezi wa 11, kwaio naomba tufatilie ili yamalizike haraka" aliongeza Kanali Sakulo.

Mkuu huyo wa wilaya amesema Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inafanya hivyo ili kuhakikisha janauari madarasa yanakuwepo ya kutosha.

Kadhalika mkuu huyo wa wilaya ametoa rai kwa madiwani wa kata zote za wilaya hiyo kushughulikia masuala ya upungufu wa matundu ya vyoo katika shule za msingi na sekondari za wilaya hiyo kwa kutoa hamasa kwa wananchi kwani changamoto hiyo ni kubwa sana.

mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo kanali Willison Sakullo


 

Post a Comment

Previous Post Next Post