" MADIWANI VITI MAALUM MANISPAA YA SHINYANGA WAFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA, TANESCO NA SHUWASA LEO ANA KWA ANA

MADIWANI VITI MAALUM MANISPAA YA SHINYANGA WAFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA, TANESCO NA SHUWASA LEO ANA KWA ANA


Na Mapuli Misalana, Shinyanga

Madiwani viti maalum wa Manispaa ya Shinyanga wamefanya ziara ya kushtukiza kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo kwenye ilani ya CCM ambapo wamefika TANESCO na SHUWASA wakiwa na lengo la kujua sababu zinazokwamisha huduma bora kwa wananchi.

Madiwani wao wa viti maalum Manispaa ya Shinyanga wametembelea na kukagua shughuli za ujenzi wa madarasa katika  shule za sekondari ikiwemo shule ya sekondari Kolandoto, shule ya sekondari Uzogore, shule ya sekondari Busulwa, shule ya sekondari Ibinzamata, shule ya sekondari Kizumbi pamoja na shule ya sekondari Mwasele ambazo zole zipo katika Manispaa ya Shinyanga.

Pia wamekagua ujenzi unaoendelea katika shule ya wasichana Bulengwa Kata ya Ndembezi, ujenzi wa Zahanati ya Lyandu kata ya Kizumbi pamoja na ujenzi unaoendelea kwenye kituo cha afya  Kambarage mjini Shinyanga.

Moja ya changamoto kubwa iliyotajwa kukwamisha shughuli hizo za ujenzi ni ukosefu wa maji pamoja na changamoto ya kukatika kwa umeme pasipo kutolewa taarifa.

Madiwa wa viti maalum Manispaa ya Shinyanga katika ziara yao wamepokea changamoto hizo ambapo wamefika kwenye shirika la umeme Mkoa wa Shinyanga TANESCO pamoja na mamlaka ya maji safi SHUWASA ikiwa lengo ni kujua sababu zinazopelekea kukosekana kwa huduma zinazotolewa na taasisi hizo.

Waheshimiwa madiwani wa viti maalum Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye shirika la umeme Mkoa wa Shinyanga walitaka kufahamu  “Tulitaka kufahamu sawa hii changamoto ya umeme ipo Nchi nzima kwa nini sisi TANESCO Shinyanga hamtuambii kuwa leo kata furani zitakosa umeme ili watu wawe wanajiandaa kwa matokeo hayo”.

Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga mhandisi Grace Tungi ametolea ufafanuzi huku akisema shirika hilo linatoa taarifa za kukatika kwa umeme kupitia mitandao ya kijamii.

“Kama ambavyo mnaelewa hivi karibuni kumekuwa na tatizo la kukatika katika kwa umeme taarifa ilishatolewa kitaifa lakini na mimi niendeleze kwa kusema kwamba tulipata changamoto ya upungufu wa maji katika mabwawa yetu na hivyo kusababisha umeme kupungua kwahiyo kutokana na tatizo hilo basi kama uzalishaji umepungua maana yake na watu kwa kipindi furani itabidi wakose umeme katika maeneo tofauti”.

“Sisi tunapata taarifa kutoka vyanzo vyetu vya umeme kwamba uzalishaji huu kwa siku utakuwa kwa kiasi gani na tunagawana  kile kinachopungua kwa mikoa yote ya Tanzania kwa Shinyanga sisi tumepata hiyo ratiba tunajua kwa kiasi gani umeme utakuwa unapungua kwahiyo tunaandaa  ratiba ya siku tano tano na tutaitangaza kwa wananchi kwamba katika siku hizo tano maeneo furani yatakosa umeme wengine watakosa asubuhi wengine watakosa umeme jioni”.amesema mhandisi Tungi

“Lakini pamoja na matangazo hayo wakati mwingine inatokea dharura kwahiyo uzalishaji ukipungua na sisi tunatakiwa kupunguza tena kwa watumiaji  na tutakuwa tunatoa taarifa katika kipindi hiki wananchi watuvumilia tu”.

 “Mgao wa umeme ni kila siku kwa Nchi nzima na kwa Shinyanga ratiba imeshaanza tunatuma kwenye mitandao ya kijamii magroup mbalimbali ya wawezeshaji lakini pia tunapeleka kwenye Radio”amesema Meneja Tungi

 Pamoja na mambo mengine madiwani wa viti maalum wamefika katika taasisi ya SHUWASA kufahamu changamoto ilayopelekea kukatika kwa maji bila kutolewa taarifa.

Akijibu maswali kaimu mkurugenzi mtendaji wa SHUWASA Reuben Mwandumbya amesema changamoto ya kukatika kwa maji inasababishwa na kukosekana kwa umeme.

“Sababu kuu ni shida ya umeme imepelekea kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa maji kwa sababu tunategemea umeme ili tuweze kuzalisha maji kwahiyo katika hizi wiki mbili kulikuwa kunashida kubwa ya mgao wa umeme Mwanza ambayo ndiyo sehemu kubwa ya maji katika mji wa Shinyanga tunapokea maji yanayotoka Mwanza kwahiyo wanapokosa umeme hawawezi kuzalisha maji”.amesema Mwandumbya

Madiwani viti maalum wa Manispaa ya Shinyanga wamelitaka Shirika la umeme TANESCO pamoja na SHUWASA kutoa taarifa za ukosefu wa huduma kwa wananchi katika Manispaa ya Shinyanga ili kumaliza kero zilizopo.

Estha Makune diwani viti maalum kata ya Shinyanga mjini, Sheila Mshandete diwani viti maalum kata ya Kambarage, Zuhura Waziri diwani viti maalum kata ya Ibadakuli pamoja na Pika Chogelo diwani viti maalum kata ya Old Shinyanga baada ya madiwani viti malum hao wa Manispaa ya Shinyanga leo wamefanya ziara ya kushtukiza kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya ilani ya chama cha mapinduzi CCM.

Madiwani viti maalum Manispaa ya Shinyanga leo wametembelea na kukagua miradi iliyopo kwenye  ilani ya CCM katika kata mbalimbali ikiwemo kata ya Kambarage, kata ya Kolandoto, kata ya Kizumbi, kata ya Ibadakuli, kata ya Ndembezi pamoja na kata Shinyanga mjini.

Waheshimiwa madiwani viti maalum Manispaa ya Shinyanga wakiwa katika ziara yao ya kushtukiza ikilenga kukagua miradi mbalimbali ya ilani ya chama cha mapinduzi CCM inayoendelea katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Waheshimiwa madiwani viti maalum Manispaa ya Shinyanga wakihoji juu ya changamoto zitokanazo na Shirika la umeme Shinyanga kwenye ofisi za TANESCO

Upande wa kulia ni diwani viti maalum kata ya Old Shinyanga Pika Chogelo akiuliza maswali kwa meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga.

Upande wa kushoto Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga mhandisi Grace Tungi akijibu maswali yaliyoulizwa na madiwani viti maalum Manispaa ya Shinyanga


Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga mhandisi Grace Tungi akiendelea kujibu maswali yaliyoulizwa na madiwani viti maalum Manispaa ya Shinyanga.

Waheshimiwa madiwani viti maalum Manispaa ya Shinyanga wakizungumza na kaimu mkurugenzi mtendaji wa SHUWASA ofisini kwake.

Diwani viti maalum kata ya Ibadakuli Zuhura Waziri kulia akiuliza maswali kwa kaimu mkurugenzi  mtendaji SHUWASA ofisini kwake.

Kaimu mkurugenzi mtendaji wa SHUWASA Reuben Mwandumbya akijibu maswali yaliyoulizwa na madiwani viti maalum Manispaa ya Shinyanga.

Diwani viti maalum kata ya Shinyanga mjini kushoto ambaye pia ni naibu meya wa Manispaa ya Shinyanga Estha Makune akizungumza na Marco Msangwa mkuu wa shule ya sekondari Kizumbi ikiwa lengo ni kupata taarifa sahihi za shughuli ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo.

Diwani viti maalum kata ya Kambarage Sheila Mshandete akishiriki katika shughuli ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye shule ya sekondari Ibinzamata.

Mkuu wa shule ya sekondari Busulwa mwalimu Gerald Majaliwa akizungumza 

Mkuu wa shule ya sekondari Busulwa mwalimu Gerald Majaliwa upande wa kulia  akizungumza na diwani viti maalum kata ya Kambarage Sheila Mshandete.

Waheshimiwa madiwani viti maalum Manispaa ya Shinyanga wakiendelea kupokea changamoto katika ziara yao.

Makamu mkuu wa shule ya sekondari Ibinzamata Selemani Hassan akieleza changamoto zinazokwamisha ujenzi wa madarasa katika shule hiyo pamoja na changamoto zingine.

Mkuu wa shule ya sekondari Uzogore Cosmas Nkoko akieleza changamoto zinazokwamisha zoezi la ujenzi wa madarasa katika shule hiyo.

Diwani viti maalum kata ya Shinyanga mjini Estha Makune upande wa kushoto akizungumza na fundi mkuu katika shule ya sekondari Kizumbi.

Waheshimiwa madiwani viti maalum Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye jengo la Zahanati ya Lyandu kata ya Kizumbi.

Waheshimiwa madiwani viti maalum Manispaa ya Shinyanga wakiendela kupata changamoto zinazokwamisha ujenzi katika miradi ya maendeleo iliyopo kwenye ilani ya chama cha mapinduzi CCM.

Mbele ni diwani viti maalum kata ya Shinyanga mjini Estha Makune wakiwa na diwani viti maalum kata ya Kambarage Sheila Mshandete kwenye zoezi la kukagua miradi ya maendeleo.

Upande wa kushoto ni diwani viti maalum kata ya Kambarage Sheila Mshandete akiwa pamoja na makamu mkuu wa shule ya sekondari Mwasele Mwalimu Maliki Yazidi Nofel.

Waheshimiwa madiwani viti maalum wakiwa kwenye kituo cha afya Kambarage  wakiendelea na ziara yao ya kushtukiza.

Mganga mfawidhi kituo cha afya Kambarage Ernest Magula akizungumza.

Waheshimiwa madiwani viti maalum wakiwa kwenye shule ya wasichana Butengwa iliyopo kata kata ya Ndembezi.

Picha katika eneo la shule ya wasichana Butengwa kata ya Ndembezi.

Diwani viti maalum kata ya Shinyanga mjini Estha Makune akishirika kwenye zoezi la ujenzi wa madarasa ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya madiwani viti maalum Manispaa ya Shinyanga.

Diwani viti maalum kata ya Ibadakuli Zuhura Waziri akishirika kwenye shughuli  ya ujenzi wa madarasa ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya madiwani viti maalum Manispaa ya Shinyanga.

Diwani viti maalum kata ya Old Shinyanga Pika Chogela akishiriki kwenye shughuli ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kata ya Ibadakuli.

TAZAMA PICHA ZOTE HAPA CHINI

 




























































































































































Post a Comment

Previous Post Next Post