"Naitwa Fareed Ismail mwarabu nimezaliwa tarehe 19 mwezi wa 11/1998 ni mtoto wa pili na wa mwisho kwa wazazi
wangu ni mzawa wa Dar es salaam pia
kiasili mimi ni Mzaramo".
"Nilianza
elimu yangu ya msingi mnamo mwaka 2006 katika shule ya msingi NDUGUMBI iliopo
magomeni DDC wengi mnaiita Makulumla kuanzia darasa la 1 paka darasa la 5
ambapo nikapata fursa ya kuhama na hapo ndipo safari yangu ya maisha ya
shinyanga ilianzia".
Nilifikia katika shule ya msingi MapinduziB hapo
ndio nilimaliza elimu yangu ya msingi kisha kujiunga na Elimu ya sekondar katika
shule ya secondary Ngokolo sec
"kiufupi katika maisha yangu yote ayo ndoto zangu ni
kua mtu maarufu kupitia nyanja ya habari kwani ni kitu nachopenda kutoka kwenye
moyo na ni ndoto yangu mtu pekee anaenifanya niipende taaluma hii ni HAMIS
MANDI(Bdozen) huyu ni kioo changu kila siku kwenye harakat zangu za kukua
kiutangazaji bado naendelea kuzipambania ndoto zangu paka nitakapo zifikia siku
moja".
Post a Comment