Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga mheshimiwa
Elias Ramadhan Masumbuko amewataka wanafunzi wanaohitimu mafunzo ya ufunzi VETA
kutokata tamaa na kwamba wanapaswa kufanya kazi pamoja na kujiajiri kutokana na
ujuzi walioupata.
Ameyasema hayo kwenye mahafali ya pili ya chuo cha
ufundi stadi Matanda Vocational Training
Centre kilichopo kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga ambapo jumla ya wanafunzi
10 wamehitimu mafunzo katika kozi
mbalimbali ikiwemo umeme pamoja na umekanika.
Mheshimiwa Elias Masumbuko ambaye alikuwa mgeni
rasmi katika mahafali hayo amewasisitiza wahitimu kufanya kazi kwa bidii kujiamini hasa pale wanapokuwa katika
shughuli zao za ujunzi waliofundishwa.
Amewakumbusha kujiendeleza zaidi ili kuwa wabobevu
wa kitaaluma kwenye ujunzi ambao wamejifunza huku akiwaasa kuondoa dhana mbaya
ya kusubiria ajira serikalini na kwamba ujunzi huo wautumie kujiajiri ili
kufikia malengo.
“Leo
mnahitimu kuna mambo ya kielimu ambayo mmekuwa mkiyapata hapa chuoni cha kwanza
mkajiendeleze huu siyo mwisho, ulimwengu wa sasa ni ulimwengu wa kiteknolojia
unamambo mengi yanayobadilika kila siku yanahitaji uelewa wa kutoka kwahiyo
msilizike sana na kiwango cha mafunzo ambayo mmekuwa mkifundishwa hapa ni vyema
sasa mkachukua hatua mkajiendeleza zaidi kutoka hapo mlipo ili kwa badae muwe
mafundi, wataalam wabobevu wa kitaaluma kwa taaluma zenu ambazo mmejifunza”.amesema
Meya Masumbuko
“Mnatakiwa
kujiamini muondoe ile hofu kile
mtakachoenda kukifanya mkifanye kwa kujiamini na siyo kwa kujaribu itakuwa ni
busara sana huko muendako kuionyesha heshima hii ambayo mmeondoka nayo hapa kwa
wazazi wenu na jamii yote inayowazunguka na kwa muonekano wenu jinsi
mnavyojituma, mkifanya kazi kwa bidii
katika utendaji wenu watatamani na wengine kuja VTC Matanda”.
“Mara
nyingine vijana wanapoteza ari wanakata tamaa anasoma akifikiri kuwa serikali
itamuajiri baada ya kukosa ajira anachoka anakata tamaa anaanza kulaumu hata
elimu aliyojifunza kwa nini tunafikia hatua kama hiyo tubadilishe mitazamo yetu
sasa kwamba kumbe tunapotoka katika elimu fundisho, elimu taaluma tunapaswa
kwenda kufanya kazi ya kujiajiri sisi kutokana na ujunzi tulioupata”.amesema
Meya Masumbuko
Aidha mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga ambaye
pia ni Diwani wa kata ya Chamaguha Mh: Elias Masumbuko amesema serikali inatoa
fursa mbalimbali ambapo kila mwananchi anapaswa kuchangamkia ikiwemo fursa ya
mikopo yenye riba nafuu inayotolewa katika kila Halmashauri kwa kuzingatia
kundi la vijana, wanawake pamoja na watu wenye ulemavu.
Kwa upande mkuu
wa chuo cha ufundi stadi Matanda Vocational Training Centre (VTC) Bwana Joaster
Thomas Kisanko akisoma taarifa fupi ya chuo ametaja baadha ya mafanikio
yaliyopo ikiwemo kujenga na kukarabati madarasa pamoja na bwani.
“Chuo
cha matanda VTC kina historia ndefu tangu Mwaka 1989 wakati wa marehemu Castory
Sekwa aliyekuwa Askofu wa jimbo katoliki
Shinyanga kwa msaada wa Misereor – Germany”.
“Mnamo
Mwaka 2010 chuo kilishindwa kupata sifa za uendeshaji mafunzo kwa mujibu wa
VETA – Taifa lakini Mwaka 2018 chuo kilifunguliwa tena na Mhasham Baba Askofu
Liberatus Sangu ambaye ni Askofu jimbo katoliki Shinyanga na kuanzishwa fani
tano ambazo tunaendelea nazo fani ya Umeme, Umekanika, Ushonaji, Uashi, Uungaji
vyuma pamoja na Udereva”.amesema Kisanko
“Sasa
hivi chuo pia kinatoa mafunzo ya Kompyuta kwa daraja la pili na kwa wale
wanaopenda programu fupi, chuo kimesajiliwa na VETA|NACTVET toka Mwaka 2019
chuo kinauwezo wa kupokea wanafunzi 540”
“Kwa
Mwaka jana 2021 chuo kilitoa mafunzo kwa wahitimu wa fani mbalimbali kama ifuatavyo
wahitimu wa udereva 97, umekanika 8, ushonaji 5, umeme 12, uungaji vyuma 2
pamoja na kozi ya Kompyuta wahitumu 14 ambapo jumla yao ni 138”.
“Historia
toka Mwaka 2018 chuo kimefundisha wanafunzi 498 wavulana wakiwa 400 na
wasichana 98, kwa muda wote chuo kimepiga hatua kubwa kujenga (Erection) na
ukarabati (Renovation) majengo ya bweni la wavulana na madarasa na karakana ya
jengo la ufundi umeme, kujenga choo na tenki”.amesema
mkuu wa chuo Kisanko
Baadhi ya wanafunzi wahitimu katika chuo hicho cha
ufundi stadi Matanda VTC wemeahidi kufanya kazi kwa bidii ili kuendana na kasi
ya mabadiliko ya teknolojia kwenye fani zao.
Wanafunzi wanaohitimu mafunzo ya ufundi katika fani
mbalimbali kwenye chuo cha Matanda Vocational Training Centre ni pamoja na John
Thomas Matemu, Ladslaus Silvest Tarimo, Mussa Ngasa Kasemele, Paskazia Ezekia
Mashiku, Pius Godwin Rwengasira, Razalo Emmanuel Dotto, Brayan Patrick Okumu,
Mathew Sylivester Mashalla. Norbert Elias Gabriel pamoja na Augustino John
Manyenye.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga mheshimiwa Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza kwenye mahafali hayo
Wahitimu wakiwa katika mahafali yao
Post a Comment