" AFISA USTAWI WA JAMII LYDIA ATOA MAAGIZO KWA SMAUJATA MKOA WA SHINYANGA

AFISA USTAWI WA JAMII LYDIA ATOA MAAGIZO KWA SMAUJATA MKOA WA SHINYANGA

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Afisa ustawi wa jamii Mkoa wa Shinyanga Lydia Kwesigabo ametoa maagizo  mbalimbali kwa viongozi wanao tekeleza kampeni ya shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga.

Maelekezo hayo ni pamoja na kufanya kazi kwa weledi, kutoa taarifa kwa vyombo husika kama polisi na ofisi za ustawi wa jamii pale wanapobaini au kupewa taarifa kuwa kunatukio la ukatili wa kijinsia au ukatili wa mtoto.

Ametoa maagizo hayo katika kikao cha pamoja cha viongozi wa serikali na viongozi wa vyuo wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine Lydia amewasisitiza kushirikiana kwa pamoja katika utekelezaji wa majukumu ya kupinga ukatili.

Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga waliohudhuria kikao hicho wameahidi kuendelea kushirikiana na kwamba watazingatia maelekezo yote yanayotolewa na viongozi wa serikali.

Aidha katika kikao hicho mratibu wa elimu ya afya kwa umma Dkt. Moses Mwita ametumia nafasi hiyo kutoa elimu juu ya kujikinga na magonjwa ya kuambukiza.

“Kila mmoja ahakikishe swala linalohusu afya alipe kipaumbele kuliko kitu chochote kwa mfano mimi hapa nimempenda binti lakini ninatakiwa nijepe kipaumbele kwamba nitapima naye kwanza ndiyo tufanya chochote tunachotaka kufanya yaani katika hili tukiweza kufanya hivi sisi sote tukaweza kujizuia kabla ya kufanya tutasaidia watoto”.

“Hayo nayasema nikiwa na maana ya kwamba tukifanikiwa kuacha ngono ndiyo tunaweza kupunguza maabukizi ya magonjwa yaani kila mmoja anapaswa kuwa na msimamo kwenye nafasi yake na ninatamani sana tubadilike katika hilo hasa sisi vijana ukitaka kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na mtu nenda kapime chukua hatua zote ili awe salama na wewe ubaki kuwa salama kwa sababu haya mambo bado yanaendelea kwenye jamii yetu na ndiyo maana maabukizi ya majowa yanaongezeka”. Amesema Dkt. Mwita

Afisa ustawi wa jamii Mkoa wa Shinyanga Lydia Kwesigabo

mratibu wa elimu ya afya kwa umma Dkt. Moses Mwita

Katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Masunga Dotto akizungumza katika kikao hicho

Kikao kikiendelea 

Kikao kikiendelea

Viongozi wa SMAUJATA wakiwa katika picha ya pamoja na afisa ustawi wa jamii mkoa wa Shinyanga Lydia Kwesigabo pamoja na mratibu wa elimu ya afya kwa umma Dkt. Moses Mwita

Post a Comment

Previous Post Next Post