Na Fabius Clavery ,Misalaba BLOG-KAGERA
Mkuu wa mkoa wa Kagera mhe.Albert Chalamila amesema
kuwa licha ya wazo la ujenzi wa kituo kubwa cha mabasi mjini Bukoba (BUKOBA BUS
TERMINAL) kuanzishwa katika kata ya Nyanga eneo la Kyakailabwa bado mkoa huo unaangalia kama eneo hilo linafaa kwa ajili ya ujenzi huo
kuendelezwa ama kuhamishiwa katika eneo jingine.
Mhe.Chalamila aliyasema hayo November 12,2022 wakati akieleza vipaumbele
vya mkoa huo kwa waandishi wa habari ambapo alisema suala la stendi serikali ya
mkoa huo inaangalia kama eneo la kwanza linafaa au kuna haja ya kutafta eneo
jipya .
“nyinyi mtakumbuka kwamba sitendi sasa
inatengenezwa pale Kyakailabwa na tayari kuna ile bilioni moja iliyokwisha
ahidiwa kwa ajili ya kuanza maandalizi ya ujenzi .Swali la msingi ni
kwamba leo hii tumeanza maandalizi ya
kutengeneza stendi yetu ya Kyakailabwa lakini swali kubwa ambalo wadau lazima
tuwashirikishe vizuri je, kati ya njia kutoka Mutukula kuingia hapa kwetu
Bukoba na kati ya njia kutoka Muleba
kuingia hapa kwetu ni ipi ina magari mengi? Kwaio majibu yawezekana
badae mkaja kuniambia kwamba inawezekana hii ya Muleba ikawa na magari mengi.
Na kwamantiki hiyo bado tunashirikisha zaidi pia watalamu kwamba pesa kubwa
hiyo itakapo kuwa imepatikana tuone je kuna haja ya kuendeleza wazo lile la
ujenzi wa stendi Kyakailabwa au tuweze kuiweka somewhere unapokaribia kuingia
mjini kwa upande unapotoka Muleba sasa hilo litakuwa ni swala mtambuka ambalo
tutawakaribisha pia wadau liweze kuwa ni suala la pamoja ili tuone kwamba sasa
tusikaribishe mzunguko ambao utakuwa hauna maana kwa wananchi wetu ” alifafanua
Chalamila mkuu wa mkoa huo.
Aliyewahi kuwa Meya wa manispaa ya Bukoba
mkoani Kagera bw,Chief Andronicus Karumuna alikiambia kituo hiki kuwa baraza la madiwani mwaka 2015-2020 liliamua kuanzisha wazo la
ujenzi wa kituo hicho cha mabasi nje kidogo ya mji katika eneo la Kyakailabwa
kwalengo wa kupanua mji huo na kodi za
watanzania zaidi ya milioni 800 zilikwishatumika katika utekelezaji wa mradi
huo ambao awakufanikisha kuukamilisha kutokana na sababu za kifedha.
“Pindi tulipounda baraza letu tulikuwa
namipango mbalimbali lakini kubwa zaidi tulikuwa naishu ya utengenezaji wa
stendi kwamaana ya kuhamisha stendi kutoka hapa ilipo na kuijenga katika maeneo
ya Kyakailabwa katika manispaa ya mji wa Bukoba katika kata ya Nyanga na
tulifanya mambo yafuatayo ya msingi, kwanza kile kiwanja ambacho kilitakiwa
kitumike kwa ajili ya masuala ya ujenzi
wa stendi ilikuwa ni ardhi iliyomilikiwa nawananchi mbalimbali wa mji wa Bukoba
kwaio swala la kwanza ilikuwa ni
kutafuta fedha ambazo zilitakiwa kwenda kufanya fidia, tulitafta hizo fedha na
tukawalipa watu waliokuwa wanamiliki hilo eneo kwa ajili ya kupisha ujenzi ”
alieleza chief karumuna aliyewahi kuwa meya wa manispaa ya Bukoba.
“kupitia fedha za ndani tuliweza kuengeneza
yafuatayo, kwanza Barabara zinzozunguka stendi ya Kyakailabwa ni takribani mita
800 kwaio katika uongozi wetu tuliacha
tumejenga mita 400 kwa kiwango cha lami kati ya mita 800 zinazozunguka kiwanja
lakini pili hatukuwa na maji pale tulipata bahati ya kuweka maji katika eneo lile, hakukuwa na umeme tulibahatika kuweka umeme hatukuwa navyoo
tukajenga vyoo Me na Ke, lakini pia tukajenga jengo la polisi ambalo kimsingi
tuliacha limekamilika, lakini pia tukajenga waiting-shave tatu kwa ajili ya abiria pamoja na kuweka parking
kwa ajili ya malori na magari mengine na ninafikiri tutakuwa tumewekeza
takribani milioni kama 900 hivi na
ushee” aliongeza Chief Karumuna.
Kadhalika Bwana Karumuna anashauri kuwa ni vyema mpango huo
undelezwe na kukamilishwa kwa ajili ya
manufaa ya wananchi wa mkoa wa Kagera.
Wilifred Rwakatale aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Bukoba
mjini anasema kuhama kwa kituo hichokutoka kilipo kwa sasa ni muhimu
na eneo lililopendekezwa linafaa zaidi kwani ni eneo ambalo kwa jiografia ya manispaa ya Bukoba
ndilo eneo ambalo alijaendelezwa na litakuwa na fursa kwa wakazi wa Bukoba na Kagera
kwa ujumla.
“huo mpango sio waleo wala jana wala juzi
kwaio tunatarajia waliopo madarakani watakamilisha huo mpango mji wa Bukoba
jinsi ulivyo kiramani hiyo stendi ingewaza kusaidia kupanua mji kwa jinsi
ilivyo kwa msingi kwamba hilo eneo ambalo walipanga liwe stendi liko nje kidogo
ya mji wa sasa na hilo eneo waliloweza kuposition liko wazi na linapakana na maeneo mengine ambayo ni makubwa
yaliyoko nje ya Bukoba”Alisema Rwakatale aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la
Bukoba mjini.
Bwana William Osward Rutta mkurugenzi wa
kampuni ya utalii ya Bukoba Tours iliyopo mjini Bukoba anasema kuwa stendi ni
fursa kubwa ya biashara na uchumi hivyo inafaa mchakato wa ujenzi wa kituo cha
mabasi cha mji huo ukashughulikiwa haraka kutokana na mkoa wa Kagera kupakana
na mataifa jirani kama Uganda Rwanda na Burundi ,anaongeza kuwa hata stendi iliyopo hivi sasa miundombinu yake
sio rafiki ukilinganisha na vituo vya
mabasi vilivyopo katika mikoa mingine hapa nchini.
“stendi ni fursa kubwa ya biashara na kiuchumi
katika sehemu yoyote ,wakati nikiwa nasafiri huwa sipendi kushuka katika
sitendi hiyo maana ni majanga matupu ,lakini kwa sababu wamekwisha sema ipo Billion
moja kwa mkandarasi sio hela ndogo ,basi
hiyo miundombinu iendelee kuwekwa . saa hizi ukifika Chato unafurahi sana
stendi ya magari madogo na makubwa inafurahisha
sana lakini ukienda Kigoma hata
stendi ya katikati ya mji unakuwa kama uko Ulaya yaani Kigoma panavutia kweli
ukienda stendi kubwa ni nzuri ukienda stendi nyingine ukienda morogoro ukienda Dodoma kwakweli unaona
nisehemu ambapo mtu unaweza ukaenda
kutalii.Kwaio ni nafasi kubwa hatujachelewa
ingawa tumechelewa kuhakikisha na
sisi tunakuwa na stendi ya kisasa yenye kukidhi mahitaji ya Tanzania na wageni
wanaotoka nchi za nje wanaokuja kutembelea mkoa wa Kagera ”alieleza bwana Osward Rutta
Mchambuzi wa masuala mbalimbali nchini
Tanzania bwana Hamuduni Maliseli Anatoa
rai kwa wataalamu waliopo ofisini katika manispaa ya Bukoba kushirikiana na
wataalamu wazawa ndani ya mkoa huo walioko mikoa Mbalimbali na maeneo tofauti ulimwenguni kujenga mji huo kisasa.
“Wamekwenda mahara wamekwenda Uswisi
wamekwenda Marekani wamekwenda Uingereza wamekwenda Ufaransa na Ujerumani wamekwenda Italia wameona watu
wanavyojenga miji inavyopangwa na kadhalika ,kwaio mimi nafikiri jambo hili
linatia aibu kubwa sana kwakweli na hasa
linapotikea kwa mji kama bukoba kwa nchi ya watu aliofanikiwa kupiga hatua ya
kimaendeleo na kifikra mapema” alieleza bwana Hamuduni
“na wale wanaokwenda Kagera viongozi kutoka
mikoa mingine wasipaone kwamba haa! wacha pawe hivyo kwa sababu sio kwetu
hapana! huko ulipokwenda ndo kwenu na sifa utakayoipata ni kule ulikofanyia kazi sio kule ulikozaliwa
kwaio mimi nafikiri ni muhimu sana kwa viongozi wa sasa”aliongeza Hamuduni
Hamad Isimaili Hamisi ni mmoja ya madereva
wanaotumia kituo cha mabasi cha Bukoba anasema hali ya kituo hicho huwa mbaya
zaidi hasa katika kipindi cha mvua lakini anaongeza kuwa kituo hicho kina eneo
dogo ambalo upelekea kufanya kazi zao kwa mazingira magumu kwani wakati
mwingine magari hukosa nafasi zakuingia na kutoka.
“changamoto kwanza tope yaani tope linatukera
alafu stendi hii inabana tunataka
angalau tuwe na stendi mbili angalau aice na kosta zijumuike sehemu moja
na mabasi yawe na stendi yake itakuwa ni
bora kwani stendi ya kyakailabwa ikiwepo nahii ikawepo iashara itakwenda vizuri
hata hapa stendi kelele zitapungua na hizi stendi zinatakiwa zisakafiwe zifanane na mikoa mingine hapa hakuna hata sehemu
ya abiria kusubiri gari unakuta wakati mwingine wamo wanarandaranda humu
ikitokea patroo ya polisi abiria
anakamatwa kama mwizi ni changamoto hakuna utaratibu ” alieleza dereva hamadi
Isimaili
Akiwa katika mkutano wa hadhara katika kata
ya Nyanga October 27,2022 mbunge wa
jimbo la Bukoba mjini ambaye pia
ni naibu waziri wa Nishati nchini Stephen Byabato alisema kuwa ujenzi wa kituo
hicho utaendelezwa muda wowote kwani tayari serikali ilikwisha idhinisha
billion moja kwa ajili ya shughuli hiyo.
“hapa tulipo ni eneo la stendi ya mabasi ya
Bukoba mjini hakuna maneno mengi mama samia alishatuhaidi atatujengea
stendi mweshimiwa makamu wa Rais
alipokuja mwezi wanne alileta ahadi ya
mweshimiwa Rais Smia na tulivyobembeleza akasema kwa kuanzia atatupatia
shilingi bilioni moja kwa ajili ya kuanzia maendeleo ya stendi yetu ndugu zangu wananyanga hili ni
eneo la stendi nay ale maswali yalikuwa yanaulizwa stendi itajengwa lini
itajengwa lini stendi itaanza kujengwa muda sio mrefu kwa sasabu tayari mama
samia amekwisha tuahidi billion moja,mradi wa stendi huu ulikuwa na vitu vinne
ndani yake niwambie vitu vingine labda
ambavyo hamvijuhi eneo hili la stendi limetengwa kwa ajili ya vitu vinne kuna
gereji hapa kuna stendi ya magari madogo kuna stendi ya magari makubwa sehemu
ya kuegesha malori kwaio kuna miradi minne ndani ya mradi mmoja.”
Ikumbukwe
kuwa mnamo Juni 9 2022,Rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania mhe.Samia
Suluhu Hassan Wakati akihutubia wananchi
wa mkoa wa kagera katika uwanja wa kaitaba alipokuwa ziarani mkoani humo
alisema“lakini mahitaji mengine mliyonayo hapa kama alivyosema mbunge wa bukoba
mjini ni soko la kisasa na stendi ya kisasahabari njema ni kwamba katika mwaka
wa fedha 2022/2023 serikali imetenga jumla ya shilingi billion moja kwa ajili
ya kuanza ujenzi wa stendi ya kisasa lakini pamoja na fedha hiyo kuna mradi unaofadhiliwa na benki ya dunia kwa
lengo la kuboresha miundombinu ya miji unaojulikana kama TACTIC kama alivyosema mweshimiwa mbunge,mradi huu utakapoanza
kutekelezwa mbali na kufadhili ujenzi wa stendi ya kisasa utafadhili pia ujenzi
wasoko kuu la manispaa ya bukoba”
Post a Comment