" MGANGA MKUU WA MKOA KAGERA DKT. ISSESSANDA KANIKI ATOA IDADI YA WATU WALIO FARIKI KWENYE JALI YA PRECISION AIR KAGERA

MGANGA MKUU WA MKOA KAGERA DKT. ISSESSANDA KANIKI ATOA IDADI YA WATU WALIO FARIKI KWENYE JALI YA PRECISION AIR KAGERA

 



Na Fabius Clavery- Misalaba Blog
Mganga mkuu wa mkoa wa kagera Dkt.Issessanda Kaniki amesema watu watatu miongoni mwa wahanga wa ajali ya ndege ya kampuni ya  Precision Air a iliyotokea mjini Bukoba mkoani Kagera mapema leo asubuhi wamefariki Dunia.

 “Tumepokea ndugu zetu watatu wakiwa wamefariki” taarifa ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Dkt. Issessanda Kaniki alieleza

Kwa mujibu wa Mganga Mkuu huyo, wawili kati ya hao waliofariki ni wanaume na mmoja ni mwanamke huku akiongeza kuwa juhudi za uokozi na msaada kwa majeruhi zinaendelea.

Awali mkuu wa mkoa wa Kagera Albart Chalamila amesema kuwa ndege hiyo ilikuwa imebeba watu wapatao 43 waudumu wawili marubani wawili na abiria 39.

Kifuatia kwa ajali hiyo Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh. Samia Suluhu Hasan ametoa pole kwa wahanga huku akitoa rai kwa wananchi kuendelea kuwa wavilivu wakati shughuli za kunusiru majeruhi zikiendelea.





Post a Comment

Previous Post Next Post