" MZEE MMOJA AUAWA USIKU KATA YA TINDE, JESHI LA POLISI MKOA WA SHINYANGA LINAMSHIKILIA MTUHUMIWA MMOJA

MZEE MMOJA AUAWA USIKU KATA YA TINDE, JESHI LA POLISI MKOA WA SHINYANGA LINAMSHIKILIA MTUHUMIWA MMOJA

 

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za mauaji ya Mzee mmoja anayefahamika kwa jina la Raphael Bundala mwenye umri wa Miaka 75 mkazi wa kijiji cha Kituli kata ya Tinde Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Jumapili majira ya saa tatu usiku  huko katika kitongoji cha Mwansami kijiji cha Kituli ambapo marehemu ameuawa kwa kukatwa na Panga sehemu mbalimbali za mwili wake.

Misalaba Blog imezungumza na Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Janeth Magomi ambaye amekili kutokea kwa tukio hilo na kwamba tayari jeshi la polisi limemshikilia mtuhumiwa mmoja kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria kuchukuliwa.

“Kwanza ni mgogoro wa ardha mzee aliyeuawa huyu alikuwa anaugomvi wa muda mrefu na mototo wa mdogo wake kijana wa kiume mzee huyu alikuwa akidai kuwa hilo shamba nila marehemu mama yake na huyu kijana naye alikuwa akidai kuwa hilo shamba alipewa na bibi yake kwahiyo mgogoro ulikuwa niwa muda mrefu”.

“Lakini usiku huo zilifanyika juhudi huyo mtuhumiwa tayari tumeshamkamata ambaye alikuwa na mgogoro wa ardhi”.amesema Kamanda Magomi

Aidha kamanda Magomi ametumia nafasi hiyo kuendelea kutoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuacha mara moja migogoro ya ardhi huku akisema jeshi hilo limejipanga kupambana na wahalifu.

“Natoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuacha mara moja migogoro ya namna hii kwa sababu tunakoelekea  kwenye mvua ndiyo hii migogoro inazidi lakini wito nikuacha mara moja na kufahamu kuwa hakuna mtu ambaye huko juu ya sheria”.

“Na sisi jeshi la polisi tumejipanga kunakikosi kazi ambacho kinafuatilia hawa wakataji mapanga na tunamafanikio tu mazuri ambayo tunauhakika tutayakomesha haya matukio”.amesema Kamanda Magomi

 

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa kijiji hicho cha Kituli Bwana Ezekiel Shija  ameeleza kuwa watu watatu wasiofahamika majina walifika katika familia hiyo usiku baada ya hapo walianza kumshambulia Mzee Raphael Bundala kwa kumkata panga na kupelekea kifo chake.

“Walikuja mabwana watatu huo usiku mzee alikuwa ndani wale watoto walikuwa bado wapo nje wanachema ni wajukuu wa marehemu baada ya kufika wale watu walimuulizia yule mzee watoto walimwita akawa ametoka nje akawaambia karibuni sasa wale watu wakamwambia sisi ni maaskari tunataka tufanye upelelezi waambie hawa watoto waende ndani tuzungumze kweli mzee aliwaambia watoto wakaingia ndani”.

“Mzee akashtuka naye baada ya kuona dalili siyo nzuri akataka kuingia ndani mmoja akamzuia akatoa panga na kuanza mumkata yule mzee akamkata sehemu ya tumbo upande wa kulia karibu na ubavu baadaye akamrudia tena nyingine akamkata shingoni mzee akaanguka pale pale huku wale watoto wakiwa wanachungulia dirishani”.ameeleza Mwenyekiti wa kijiji Bwana Shija

Marehemu mzee Raphael Bundala alikuwa akiishi kwake na familia yenye watoto sita (6) na kwamba mazishi yatafanyika leo majira ya saa kumi jioni katika kitongoji cha Mwansami kijiji cha Kituli kata ya Tinde mkoani Shinyanga.

 

 

 

Post a Comment

Previous Post Next Post