Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa polisi Janeth Magomi amekemea watu wenye mamlaka ya uongozi kutumia nafasi zao kutaka rushwa ya Ngono.
Kamanda Magomi ameyasema hayo wakati akizindua kampeni ya kupambana na
rushwa ya ngono iliyofanyika katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga.
Kampeni hiyo inaendeshwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Karibu
Tanzania Organization (KTO) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa (TAKUKURU) na Vyuo 54 vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs) huku ikiwa imebeba
ujumbe wenye kauli mbiu isemayo ‘ Kuwa Jasiri Kataa Rushwa
ya Ngono’
Amesema wapo baadhi ya watu wanaotumia vibaya
mamlaka waliyonayo katika kutoa huduma za jamii , kwa kutaka rushwa ili kutoa
huduma hizo, jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo hasa katika kukabiliana
na vitendo vya ukatili na mapambano dhidi ya rushwa.
Kamanda Magomi amesema rushwa ya ngono ni moja ya tatizo
linaloonekana ,kuwa sehemu ya baadhi ya watu kutumia vibaya madaraka na nafasi
walizonazo , kushawishi watu ili waweze kupata huduma na haki hizo, jambo
ambalo ni ukatili unaopaswa kukemewa na kila mtu, kwa kupingwa kwa nguvu zote,
kwani ni kinyume cha sheria.
Amesema matumizi mabaya ya mamlaka ni kuendeleza
videndo vya ukatili ambapo ametaja athari za rushwa ya ngono huku akiwasihi
wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuendelea kushirikiana na serikali kupitia idara
zake kama vile jeshi la Polisi pamoja na TAKUKURU ili kutokomeza vitendo vya
rushwa ya ngono.
“Rushwa
ya ngono ni kitendo cha mtu mwenye mamlaka au madaraka kumshawishi mtu kutoa
mwili wake kingono ili aweze kupata huduma au haki lakini sheria ya kuzuia na
kupambana na rushwa namba 11 ya Mwaka 2007 inakataza mtu yoyote mwenye mamlaka
kutumia mamlaka aliyonayo katika kutekeleza majukumu yake kwa kudai au kulazimisha
upendeleo wa kingono”.amesema Kamanda Magomi
“Watu
wenye mamlaka viongozi katika ngazi mbalimbali kwenye jamii hutumia fursa hiyo
kufanyia wanawake zuruma ya kingono lakini pia katika vyuo mashuleni walimu
hushawishi wanafunzi kufanyanao ili wapate maksi za juu lakini katika vyombo
vya sheria mtu hutakiwa kutoa rushwa ya ngono asaidiwe ili asichukuliwe hatua
dhidi ya kesi inayomkabili”.amesema kamanda Magomi
“Rushwa
ya ngono ni kitendo cha ukatili, athari zake rushwa ya ngono inaua kwani ni
chanzo cha kusambaza magonjwa, pili rushwa ya ngono inazalilisha na kusababisha
msongo wa mawazo tatu rushwa ya ngono inanyima haki za wenye haki na kumpa haki asiyestahili nne
rushwa ya ngono inasababisha Taifa kuwa na watumishi kwenye sekta na idara zote
wasiostahili”.amesema kamanda Magomi kwenye uzinduzi
wa rushwa ya ngono Mkoani Shinyanga
“Kunyamazia
vitendo vya rushwa ya ngono ni kukuza na kueneza tatizo na hivyo kuongeza
uzalilishaji na ukatili kwa watoto wetu, mama zetu, ndugu jamaa na marafiki wito
weto kwa wananchi ni kuendelea kuvunja ukimya kupaza sauti ili kwa pamoja
tuweze kutokomeza vitendo hivyo”. Amesema Kamanda Magomi
Mkurugenzi wa
wa shirika lisilo la kiserikali la Karibu Tanzania Organization (KTO) Maggid
Mjengwa amesema uwepo wa vitendo vya rushwa ya ngono inatokana na mmomonyoko wa
maadili pamoja na tamaa za kujipatia mali katika jamii.
Mjengwa amesema mmomonyoko wa maadili unaotokana na
baadhi ya watu kutaka kujipatia mali kwa njia zisizo halali, hususani kuomba au
kutoa rushwa ya ngono katika kupata au kutoa huduma kwa jamii, ni sababu
inayochangia uwepo wa vitendo vya ukatili na rushwa ,jambo ambalo ni kikwazo
cha maendeleo ya familia na Taifa kwa ujumla.
Amesema kuendelea kwa vitendo hivyo vinasababisha
kuwepo kwa athari mbalimbali katika jamii hivyo kila mwananchi anapaswa kupambana dhidi ya vitendo hivyo ili
kuepuka athari.
“Watu
kukosa maadili ndiyo moja ya chanzo cha vitendo vya rushwa kuna fikira katika
jamii kwamba tendo likitokea anasema hilo halinihusu mimi nilakwao kwa mfano
mtu anachukua pesa kwa rushwa na daraja anajenga kwa kiwango cha chini halafu
unasema hilo jambo halinihusu ni kazi ya TAKUKURU tubadilishe fikra tuepuke athari hizo”.amesema
Mkurugenzi wa KTO Mjengwa
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya
Shinyanga, mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii Manispaa ya Shinyanga John
Tesha amesema vitendo vya rushwa
vinachangia utekelezaji mbaya wa miradi mbalimbali ya maendeleo Nchini ambapo
amesisitiza kwa jamii kutoa taarifa
wanapobaini viashiria ama vitendo vya rushwa.
Tesha amesema vitendo vya rushwa vinachangia
kurudisha nyuma shughuli za maendeleo katika jamii kutokana na kukosa haki na huduma bora , na hivyo kuwataka
wananchi kushirikiana na mammlaka zinazohusika, kutoa taarifa pindi wanapobaini
viashiria ama vitendo vya rushwa ili
kutokomeza vitendo hivyo.
“Tukiwa
na jamii ambayo inakataa rushwa maana yake hiyo ni jamii inayojitambua na ni
jamii ambayo itakuwa na maendeleo tuendelee kusisitiza sehemu mbalimbali za
kazi pamoja na maeneo mengine ya utoaji huduma rushwa isiwepo kama kuna yoyote
basi fika sehemu husika ili jambo hilo liweze kushughulikiwa kwa haraka”.
“Maendeleo
hayawezi kuwa endelevu kama kutakuwa na rushwa, rushwa inafanya mradi usiwe
imara kwa maana mradi utachakachuliwa lakini kama hakuna rushwa huo mradi
utakuwa imara na utatoa huduma iliyotarajiwa tuwaomba wananchi tuendelee
kushirikiana katika kupambana na rushwa ya ngono”.amesema
Bwana Tesha
Akizungumza kwa niamba ya Mwenyekiti wa bodi ya KTO
ambaye ni mkuu wa chuo cha maendeleo ya wananchi Mtawanya (FDC) kilichopo Mkoa
wa Mtwara Mshana Halfan amesema shirika hilo linaendeleo na jitihada mbalimbali
za kukabiliana na mapambano dhidi rushwa ya ngono.
Halfan amesema vyuo 54 vya Maendeleo ya Wananchi vimeendelea kushirikiana na KTO na TAKUKURU kutoa elimu ya kupinga rushwa ya ngono kwa kuendesha Programu mbalimbali ikiwemo Programu ya Elimu Haina Mwisho ambayo ni Programu maalumu ya kuendeleza maarifa kwa wanawake vijana waliokatishwa masomo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ujauzito pamoja na wale ambao hawakupata nafasi ya kuendelea na masomo ya sekondari, watasoma masomo ya sekondari kupitia mfumo usio rasmi, masomo ya ufundi, ujasiriamali na stadi za maisha bure.
Kwa upande wake Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Mwamba
Masanja, amesema rushwa ya ngono siyo fursa ya kujinufaisha ambapo amewataka
wananchi kutoa taarifa za rushwa ya ngono ili wahusika waweze kukamatwa na
kuchukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa lengo ni kutokomeza vitendo vya rushwa
ya ngono.
Naye Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi, Maria Mkanwa amesema
chuo hicho pamoja na vyuo vingine vya maendeleo ya wananchi kwa kushirikiana na
KTO wameendelea kutoa elimu ya kupinga
rushwa ya ngono pamoja na kutoa Proramu mbalimbali kwa ajili ya kuwawezesha
wananchi hasa kundi la wanawake.
Uzinduzi
wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono umefanyika Jumamosi Desemba 17,2022
katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga ukiambatana na utoaji wa elimu
ya Rushwa ya Ngono kwa njia mbalimbali ikiwemo michezo ya Baiskeli ambapo
washindi wote waliofanya vizuri katika michezo hiyo wamepewa zawadi.
Kampeni ya
kupambana na rushwa ya ngono imeandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la
Karibu Tanzania Organization (KTO) kwa
kushirikiana na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa
Shinyanga na Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Buhangija ambapo imekwenda
sanjali na kauli mbiu isemayo “KUWA JASIRI KATAA RUSHWA YA NGONO”.Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa polisi Janeth Magomi akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya kupinga rushwa ya ngono Mkoani Shinyanga.
Mkurugenzi wa wa shirika lisilo la kiserikali la Karibu Tanzania Organization (KTO) Maggid Mjengwa akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupinga rushwa ya ngono Mkoani Shinyanga.
Mkurugenzi wa wa shirika lisilo la kiserikali la Karibu Tanzania Organization (KTO) Maggid Mjengwa akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupinga rushwa ya ngono Mkoani Shinyanga.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, ambaye ni mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii Manispaa ya Shinyanga John Tesha akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya kupinga rushwa ya ngono Mkoani Shinyanga.
Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Mwamba Masanja akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kupinga rushwa ya ngono Mkoani Shinyanga
Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Mwamba Masanja akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kupinga rushwa ya ngono Mkoani Shinyanga
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa bodi ya KTO ambaye ni mkuu wa chuo cha maendeleo ya wananchi Mtawanya (FDC) kilichopo Mkoa wa Mtwara Mshana Halfan akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kupinga rushwa ya ngono Mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi, Maria Mkanwa akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya kupinga rushwa ya ngono Mkoani Shinyanga.
Mtoa huduma za
kisheria ngazi ya jamii, Anne Deus kutoka kituo cha Msaada wa Kisheria
Community Edivication Organization (CEO) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya
Ngono Mkoani Shinyanga.
Uzinduzi wa kampeni ya kupinga rushwa ya ngono Mkoani Shinyanga imehudhuriwa na viongozi kutoka Mikoa mbalimbali za hapa Nchini wakiwemo wakuu wa vyuo vya maendeleo ya wananchi (FDC).
Viongozi mbalimbali wamehudhuria uzinduzi wa kampeni ya kupinga rushwa ya ngono, viongozi hao ni pamoja na mkuu wa chuo cha maendeleo ya wananchi (FDC) Malya Bwana Frenk Igembe, mkuu wa chuo cha FDC Mtawanya Bwana Mshana Halfan, Mkuu wa chuo cha FDC Sikonge Bwana Enock Lalida , Bwana Hagau Shila mkuu wa chuo cha FDC Sengerema, Bwana Gerald Tesha mkuu wa chuo cha FDC Masasi, Bwana Elias Kulmay mkuu wa chuo cha FDC Urambo, Bwana Ramadhan Simba mkuu wa chuo cha FDC Kasulu, pamoja na Faraji Mwadua mkuu wa chuo cha FDC Mwambala.Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa polisi Janeth Magomi akiwa katika zoezi la kukabidhi zawadi kwa washindi wa mbio za Baskeli.
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa polisi Janeth Magomi akiwa katika zoezi la kukabidhi zawadi kwa washindi wa mbio za Baskeli.
TAZAMA PICHA ZOTE HAPA CHINI
Post a Comment