" MAGEREZA SHINYANGA WAMEITUMIA VYEMA SIKU YA UHURU WA TANGANYIKA

MAGEREZA SHINYANGA WAMEITUMIA VYEMA SIKU YA UHURU WA TANGANYIKA

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Magereza Josephine Semwenda na Mkuu wa Gereza  la Wilaya ya Shinyanga William Makwaya kwa kushirikiana na maaskari wao wameadhimisha Miaka 61 ya uhuru wa Tanganyika kwa kufanya usafi wa Mazingira katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Shinyanga.

Shughuli hiyo ya usafi wa Mazingira imefanyika leo Disemba 9, 2022 majira ya Asubuhi ikiwa ni kilele cha siku ya Uhuru wa Tanganyika kutimiza Miaka 61 hapa Nchini.

Akizungumza baada ya kushirika shughuli hiyo, Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Shinyanga William Makwaya amesema wamehamasika kuungana na watanzania wengine kuitumia vyema siku hii kwa kushirika shughuli mbalimbali ikiwemo kufanya usafi wa Mazingira.

Aidha Mkuu huyo amesema katika eneo lao tayari wameshapanda miti zaidi ya Elfu kumi  kwa lengo la kupendezesha mazingira ya Mji wa Shinyanga.

“Tumeadhimisha siku hii kwa kufanya usafi katika eneo letu tumefanya usafi kambini, tumeufanya katika uwanja wetu wa mazoezi lakini pia tumefanya usafi katika msikiti uliopo karibu na magereza kwa ujumla tumesherehekea vizuri na tumehamasika kujua kwamba tuko pamoja na serikali yetu katika kuhakikisha kwamba kila kitu kinakwenda kulingana na taratibu, sheria na kanuni”.amesema Makwaya

“Mkoa wetu wa Shinyanga unahitaji sana kupanda miti ili turudishe uoto wa asili na sisi kama magereza tumehamasika na tumepanda miti zaidi ya Elfu kumi kuzunguka eneo letu na tunaitunza tunahakikisha kwamba baada ya miaka kadhaa itakuwa imefikia hatua ya kutoa kivuli na matunda kwa lengo la kuibadilisha kuwa Shinyanga ya kijani”.amesema Mkuu wa Gereza Wilaya ya Shinyanga Makwaya

Leo Disemba 09,2022 watanzania wameadhimisha kumbukumbu ya Miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara,ambapo Mkoa wa Shinyanga nao umeungana na Mikoa Mingine kwa kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo usafi wa mazingira.Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Magereza Josephine Semwenda akishiriki shughuli ya usafi.Mkuu wa Gereza  la Wilaya ya Shinyanga William Makwaya.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Magereza Josephine Semwenda na Mkuu wa Gereza  la Wilaya ya Shinyanga William Makwaya wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumaliza zoezi la kufanya usafi wa Mazingira.TAZAMA PICHA ZOTE HAPA CHINI








 

Post a Comment

Previous Post Next Post