" PADRE MSABILA AWAKUMBUSHA WAZAZI NA WALEZI KUSHIRIKIANA NA WALIMU, MAHAFALI YA 24 ST. MARY’S DAY CARE MWADUI.

PADRE MSABILA AWAKUMBUSHA WAZAZI NA WALEZI KUSHIRIKIANA NA WALIMU, MAHAFALI YA 24 ST. MARY’S DAY CARE MWADUI.

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Paroko wa parokia ya Mwadui Padre Michel Msabila amewakumbusha wazazi na walezi kushirikiana na walimu katika malezi ya watoto shuleni ili waweze kukua katika mazingira ya uadilifu zaidi.

Ametoa mafundisho hayo wakati akihubiri kwenye adhimisho la misa takatifu ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya wanafunzi wahitimu wa shule ya awali ya St. Mary’s day care iliyofanyika kwenye kanisa la Msalaba Mtakatifu Parokia ya Mwadui,Wilayani kishapu Mkoani Shinyanga

Amewasisitiza wazazi na walezi kuwekeza kwenye elimu ya watoto wao kama msingi wa kuwaandaa ili waweze kukabiliana na mazingira ya Dunia ya sasa inayotaka wasomi.

Padre Msabila ambaye pia ni meneja wa shule hiyo amewataka wanafunzi wahitimu kuongeza juhudi za kujifunza ikiwa ni pamoja na kuwaheshimu walimu, wazazi na walezi ili kufikia malengo waliyokusudia

Akizungumza Mkuu wa shule ya awali St. Mary’s day care Deusdedith Malale amesema Mwaka huu 2022 shule imefanya mahafali ya 24 tangu kuanzishwa kwake ambapo  wanafunzi 36 wamehitimu masomo yao ya awali.

Aidha mkuu huyo wa shule  amesema shule hiyo inatoa mafunzo ya dini kwa nadharia na vitendo kama chanzo cha maarifa na kutoa elimu bora hivyo amewaomba wazazi na walezi kupeleka watoto wao katika shule hiyo ili waweze kukua katika misingi yenye maadili yanayompendeza Mungu.

Kwa upande wao baadhi ya watoto wahitimu katika shule ya awali St. Mary’s day care  centre Mwaka huu 2022 wamemshukuru Mungu kwa kuhitimu huku wakitoa ahadi zao juu ya elimu yao kuwa wataendeleza juhudi zao ili kuimarika zaidi kitaaluma.

 

Paroko wa parokia ya Mwadui Padre Michel Msabila akihubiri kwenye adhimisho la misa takatifu ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya wanafunzi wahitimu wa shule ya awali ya St. Mary’s day care  



TAZAMA PICHA ZOTE HAPA CHINI











 

Post a Comment

Previous Post Next Post