Chama
cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini
kimezindua kampeini za uchaguzi mdogo wa nafasi ya udiwani katika kata
ya Mwamalili,Jimbo la Uchaguzi la Shinyanga Mjini.
Akizindua
kampeni hizo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Mabala Mlolwa amewaomba
wakazi wa kata hiyo kumchagua mgombea wa CCM Bwana James Mdimi ili aweze
kuwasaidia kutatua changamoto zilizopo
katika kata hiyo.
Mwenyekiti
huyo amesema iwapo Mdimi atachaguliwa atatumia nafasi yake kushirikiana na
viongozi wengine wa chama na serikali kuhakikisha ilani ya uchaguzi
inatekelezwa kikamilifu.
“Wana Mwamalili wakiwemo wa Bushola
na vijiji vingine niwaombe sana siku ya Jumamosi mkampigie kura Mdimi mtakuwa
mmeenda vizuri niwaombe mjitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura na kura hakuna kwingine zote tumpigie
Mdimi”.amesema
Mlolwa
“Mdimi ni mgombea wa chama cha
mapinduzi atasimamia ilani ya chama ambayo imeainishwa mambo yapi ya kufanya yamo Mdimi atashirikiana na wenzake
madiwani kuhakisha Mwamalili mahitaji yenu mnayoyataka yanakuja kwa uharaka
zaidi”.amesema
Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mabala
Akizungumza
katika kampeni hiyo mgombea wa nafasi ya udiwani kata ya mwamalili Bwana James Mdimi amewaomba wananchi kumchagua ili aweze kutatua
changamoto zilizopo, ambapo amevitaja vipaumbele vyake iwapo atachaguliwa,kuwa
ni pamoja na kushughulikia changamoto ya umeme na Maji.
“Mimi ni mwenyeji wa hapa Geographia
ya kata ya Mwamalili naifahamu vizuri sana kwahiyo najua Bushola kuna shida
gani, Seseko kuna shida gani na Mwamalili kuna shida gani hapa Bushola shida
kubwa ni maji ya Victoria lakini pia umeme na vipaumbele vyangu ni maji, umeme,
elimu na afya”.amesema
Mdimi
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mheshimiwa Elias Ramadhan Masumbuko akiwawakilisha
madiwani wengine amewaomba wakazi wa kata ya Mwamalili kumchagua James Mdimi katika nafasi ya udiwani kata ya Mwalili ili
aweze kushughulikia changamoto zilizopo.
Aidha
viongozi mbalimbali wa ngazi ya Mkoa na wilaya wametumia nafasi hiyo kuwaomba
wananchi wa kata ya Mwamalili kumchagua James Mdimi katika
nafasi ya udiwani kata hiyo.
Kwa
upande wao baadhi ya wananchi wa kata ya Mwamalili wamesema wanahitaji mgombea
mwenye sifa za uongozi ambaye ataweza kuishnikiza serikali kutatua changamoto
na kero zilizopo hali itakayochangia ustawi na maendeleo ya wananchi.
Uchaguzi
huo mdogo wa nafasi ya udiwani katika kata ya Mwamalili unafanyika kuziba pengo
la aliyekuwa diwani wa kata hiyo Paulo Machela ambaye alifariki Dunia Mwanzoni
mwa Mwaka huu 2022.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Mabala Mlolwa akizungumza kwenye kampeni kijiji cha Bushola kata ya Mwamalili.
Mgombea wa nafasi ya udiwani kata ya mwamalili Bwana James Mdimi akipandishwa jukwaani kwa ajili ya kuzungumza na wakazi wa kata ya Mwamalili.
Katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Said Bwanga akizungumza kwenye kampeni hiyo.











Post a Comment