Askofu wa kanisa la Africa Inland Church
Tanzania AICT Dayosisi ya Shinyanga Zakayo Bugota amewakumbusha
wakristo wajibu wa kutumia karama mbalimbali kuchochea maendeleo na ustawi wa
kanisa na jamii ili kutimiza mapenzi ya Mungu.
Amesema kila mmoja kwa nafasi yake amebarikiwa
karama ya aina yake ikiwemo taaluma, vipaji na maarifa hivyo ni vyema kutumia
nafasi hiyo kutengeneza alama itakayodumu kizazi hadi kizazi.
Askofu Bugota ameyasema hayo leo Januari 15,2023 wakati
akihubiri katika ibada ya Jumapili kwenye kanisa la AICT Kambarage mjini
Shinyanga ambapo amesisitiza wakristo kutumia utume wao kwa lengo la kuchochea
maendeleo na ustawi wa kanisa na kuwanufaisha wengine kama ishara ya kutii
mapenzi ya Mwenyezi Mungu.
Amesema wakristo wanapaswa kutumika na kuacha alama
zenye kumbukumbu za kimungu ambazo ni matokeo chanya katika jamii na Taifa kwa
ujumla.
Askofu Bugota ambaye pia ni makamu mkuu wa Askofu
kanisa la AICT amewasisitiza waumini wa kanisa hilo kuishi maisha
yanayompendeza Mungu ili waweza kubarikiwa siku hadi siku.
Misalaba Blog imezungumza na baadhi ya waumini wa
kanisa hilo ambao wamempongeza askogu Bugota kwa mahubiri hayo huku wakiwaomba
wakristo wengine kutumia vipaji vyao kuleta matokeo chanya katika jamii.
waumini hao pia wameahidi kuendelea kuzingatia mafundisho
yanayotolewa na viongozi wa kanisa hilo ikiwa ni pamoja na kujitoa zaidi
kumtumikia Mungu ili waweze kubarikiwa kizazi hadi kizazi.
Post a Comment