Emmanuel Mathias, maarufu kama MC Pilipili, mshereheshaji na msanii wa uchekeshaji nchini Tanzania, amefariki dunia ghafla leo mchana, Novemba 16, 2025.
Taarifa zinaeleza kuwa, MC Pilipili alisafiri kuelekea jijini Dodoma ambapo jioni ya leo alitarajiwa kwenda kufanya kazi yake ya ushereheshaji jijini humo, lakini akafikwa na mauti.
Chanzo kimoja kimezungumza na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya General, Dodoma, Ernest Ibenzi ambaye amethibitisha taarifa hizo na kueleza kuwa MC Pilipili amefikishwa hospitalini hapo akiwa tayari amefariki dunia.

Chanzo - GOLD FM TANZANIA
Post a Comment