" BURUTE SACCOS LTD YAENDELEA NA MIKUTANO YA WANACHAMA NGAZI YA KATA, YAELEZA MAENDELEO NA MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU 2025

BURUTE SACCOS LTD YAENDELEA NA MIKUTANO YA WANACHAMA NGAZI YA KATA, YAELEZA MAENDELEO NA MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU 2025

Na Lydia Lugakila, Misalaba Media BukobaChama cha ushirika cha akiba na mikopo kilichosajiliwa kwa lengo la kukusanya akiba kutoka kwa wanachama na kutoa mikopo kwa riba nafuu kwa wanachama kijulikanacho kama BURUTE SACCOS LTD  kimefanya mkutano wa wanachama ngazi ya kata katika ukumbi wa KCU uliopo Manispaa ya Bukoba, ikiwa ni mwendelezo wa mikutano yake ya kata inayolenga kuwafikishia wanachama taarifa muhimu za chama na kupokea maoni ya ujenzi kwa ajili ya kuboresha utendaji.Mkutano huo umefanyika Novemba 16, 2025 na kuhudhuriwa na wanachama kutoka maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Bukoba, ambapo viongozi wa BURUTE SACCOS LTD waliwasilisha taarifa ya maendeleo ya chama, maendeleo ya fedha, miradi ya kiuchumi, na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka uliopita.Aidha,bodi imewasilisha taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Mkutano Mkuu wa mwaka 2024, ikionyesha namna maamuzi ya wanachama yalivyofanyiwa kazi, haswa kwenye maeneo ya uwekezaji, uboreshaji wa huduma, na ukusanyaji wa fedha za chama.Vilevile, uongozi wa SACCOS umewataka wanachama kuendelea kutoa maoni na mapendekezo yatakayotumika katika maandalizi ya Mkutano Mkuu wa mwaka 2025, ili kuhakikisha kuwa sauti ya kila mwanachama inafika na kuchangia katika maendeleo ya taasisi.Kwa mujibu wa ratiba, mikutano ya ngazi ya kata itaendelea Novemba 22, 2025 katika kituo cha Lyamahoro Shule ya msingi na Novemba 23 mwaka huu katika kituo cha Mugana “B” shughuli ambapo wanachama wa maeneo hayo nao watapata fursa ya kujadili mwenendo wa chama na kutoa maoni yao.Uongozi wa BURUTE SACCOS LTD umeendelea kusisitiza umuhimu wa ushiriki wa wanachama katika mikutano hii, kwa kuwa ni chombo muhimu cha uwajibikaji, uwazi, na kuboresha ustawi wa wanachama wote.


Post a Comment

Previous Post Next Post