" CHADEMA MKOA WA SHINYANGA KUANZA MIKUTANO YA HADHARA MWENYEKITI NTOBI AWAKARIBISHA WANANCHI MWANZA UZINDUZI WA KITAIFA

CHADEMA MKOA WA SHINYANGA KUANZA MIKUTANO YA HADHARA MWENYEKITI NTOBI AWAKARIBISHA WANANCHI MWANZA UZINDUZI WA KITAIFA

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Bwana Emmanuel Ntobi amesema  Chama hicho  kitaanza Mikutano ya hadhara  Mwezi Februari Mwaka huu ambapo uzinduzi  wake utafanyika katika Manispaa ya Shinyanga

Amesema     uzinduzi huo utatanguliwa na uzinduzi wa  kitaifa utakaofanyika  kanda ya Victoria  katika viwanja vya furahisha jijini Mwanza  ambapo mgeni rasmi atakuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Bwana Freeman Mbowe.

Amefafanua zaidi kuwa uzinduzi mwingine wa kanda ya Serengeti inayojumuisha Mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara utafanyika katika Musoma Mkoani Mara.

“Mkoa wa Shinyanga tumejipanga kuanza mikutano yetu ya hadhara Mwezi wa pili tutaanza kuzindua katika Manispaa hii ya Shinyanga badae Kahama na majimbo mengine Ushetu, Msalala, Solwa na Kishapu kwa sasa hivi tunasubiri kwanza ufanyike uzinduzi wa Kitaifa ambapo utafanyika katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza ambapo Mwenyekiti wa chama Freeman Mbowe ndiyo mgeni rasmi lakini pia tutaenda kuzindua katika kanda yetu ya Serengeti kwa mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu ambapo uzinduzi utafanyika Mkoa wa Mara Musoma mjini katika viwanja vya shule ya Kindwa na mkutano utaanza asubuhi saa mbili hadi saa kumi na mbili jioni”.amesema Mwenyekiti Ntobi

Amesema CHADEMA itafanya Mikutano yake kwa kuzingatia katiba na sheria za Nchi, kuuza sera ,kutumia majukwaa kidemokrasia kueleza sera mbadala,na ajenda zinazolenga kuwasilisha hoja za kusaidia Wananchi.

Ntobi amewaomba Wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kufika kwenye mikutano hiyo ama kufuatilia kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii,ili kuwasikiliza viongozi wa chama hicho wakielezea sera na ajenda muhimu zinazolenga kuishinikiza serikali kuwakwamua wananchi kutoka kwenye hali ngumu ya Maisha.

Hatua hiyo ya CHADEMA ni utekelezaji wa tamko la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amerusu Mikutano ya hadhara kwa vyama vya Siasa Nchini.

Post a Comment

Previous Post Next Post