Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi ya Chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga John Siagi amesema Miaka 46 ya CCM viongozi wa jumuiya hiyo wawe na utaratibu wa kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Ameyasema hayo leo baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa soko la mitumba katika kata ya Ngokolo na ujenzi wa shule ya sekondari ya bweni ya wasichana Butengwa kata ya Ndembezi, miradi inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Bwana Siagi amesema kwa kufanya hivyo itasaidia kutatua kero za wananchi na kupunguza changamoto zilizopo hivyo kuchochea ustawi na maendeleo kwa wananchi.
“Chama hiki shabaha yake kubwa ni kuziishi kero za wananchi kipindi cha nyuma wananchi walikuwa wakipata changamoto ama kero walikuwa wanazipeleka kwa viongozi wa chama leo viongozi wa chama nao baadhi yao wamekuwa ni sehemu ya kulia kero wakati wao ndiyo wenye wajibu wa kuisimamia serikali”.
“Niwashauri viongozi wenzangu tengeni muda wa kufuatilia kero kwa sababu serikali hii tunaisimamia sisi kama kiongozi ukishindwa kutatua kero za wananchi vipo vikao maalum ndani ya chama vitashughulikia msisubirie viongozi watoke ngazi ya juu”.amesema Mwenyekiti Siagi
Siagi amewataka wanachama wa Jumuiya hiyo na chama cha mapinduzi kwa ujumla kushirikiana na wabunge na madiwani waliopo madarakani ili waweze kutekeleza vyema ilani ya CCM kwa kushirikiana na serikali.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Fue Mrindoko amewataka wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuhakikisha wanawalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili.
“Maadili yamevurugika mpaka kwa watoto wetu wa miaka ya chini miaka saba miaka kumi hakuna malezi tena ni uovu tu lakini sisi wazazi ndiyo tunatakiwa tuwalee maana ulawiti umeongezeka kwa watoto wetu lakini wazazi tupo na wakati mwingine wazazi tunafahamu kabisa kuwa mtoto wangu amelawitiwa akipelekewa shiringi elfu ishirini anaona ni vyema kumuangamize mototo ili huyo mharifu asichukuliwa hatua za kufungwa maisha mimi , tupinge vitendo hivyo kwa sauti moja tukiona kunauharufu wa namna hiyo ni vyema tukatoa taarifa sehemu husika na kwa uharaka”.amesema
Naye mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Anord Makombe amepongeza jitihada za serikali katika miradi hiyo huku akiwasisitiza wananchi kutunza miundominu ya miradi hiyo.
Katibu itikadi, siasa na uenezi Wilaya ya Shinyanga mjini Said Bwanga amewakumbusha viongozi na wanachama wa CCM Wilaya hiyo kutokuwa na makundi na kwamba wanapaswa kuwa na umoja katika utekelezaji wa majukumu yao.
Awali wakati viongozi hao wakitembelea na kukagua miradi hiyo wameuliza maswali mbalimbali wakitaka kujua taarifa sahihi katika utekelezaji wa miradi hiyo miwili ambapo kaimu mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Bwana John Tesha wakati akielezea ujenzi wa soko la mitumba kata ya Ngokolo amesema mradi huo unatarajiwa kukamilika Februari 28,2023.
“Mradi huu ulianza tarehe moja mwezi wa 11 Mwaka 2022 na unatarajiwa kukamilika tarehe 28, mwezi wa pili mwaka 2023 mradi huu unagharimu shiringi jumla ya Milioni Mia nne na themanini ambapo hapa kutakuwa na wafanyabishara zaidia ya Mia mbili”.amesema Tesha
Naye afisa elimu sekondari Manispaa ya Shinyanga Lucas Mzungu wakati akisoma taarifa ya ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo kata ya Ndembezi amefafanua hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ujenzi wa majengo ya shule hiyo.
“Vyumba vya madarasa 12 ambapo vyumba 6 vyenye ofisi viko katika hatua za ukamilishaji pia vyumba viwili vyenye vyoo na vyumba 4 viko hatua za ukamilishaji, maabara za Fizikia, Jiografia, Kemia na Biolojia vimekamilika na kuezekwa pamoja na kupigwa ripu kuna vyoo matundu 16 vimejengwa na kupigwa ripu lakini kuna mabweni 5 pia yamejengwa na ujenzi wa bwalo unaendelea kwa kuinua kuta pande zote lakini kuna jingo la utawala tayari limekamilika pamoja na nyumba mbili za walimu zimejengwa na zipo kwenye hatua ya ukamilishaji”.
“Mradi huu ulitarajiwa kukamilika na kuchukua wanafunzi mwezi Desemba Mwaka 2022 hadi sasa shule imeshasajiliwa changamoto iliyopo ni baadhi ya majengo na miundombinu mingine bado haijakamilika pindi itakapokamilika wanafunzi watakaopokelewa niwa kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanga”.amesema afisa elimu Mzungu
Aidha akizungumzia ziara hiyo katibu wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga mjini Doris Yotham Kibabi ameeleza kuwa wamepanda miti zaidia yay a mia mbili ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya wazazi kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi CCM.
Jumuiya ya Wazazi ya chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini leo imetembelea na kukagua miradi miwili ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 46 ya kuzaliwa kwa chama hicho.
Shughuli hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na viongozi wa CCM wakiwemo viongozi wa umoja wa vijana Wilaya ya Shinyanga mjini.
Post a Comment