
Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mwanamke anayefahamika
kwa jina la Scholastica Peter mwenye umri wa Miaka 28 mkazi wa mtaa wa Bugwandege kata ya
Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga, amewajeruhi watoto wake wawili kwa kuwachoma
moto mikononi kwa kile alichodai alikuwa akiwaonya baada ya kukomba mboga.
Misalaba Blog imefika na
kuzungumza na Mama huyo ambaye amekiri kuwachoma moto watoto hao, akisema alifanya hivyo kama hatua ya kuwaonya, kwa sababu wana tabia ya udokozi wa mboga
“Hawa
watoto wanatabia ya udokozi ile siku nilipika mboga tukala usiku tukaibakiza asubuhi
nikatoka nikaenda kutembeze mboga nikakuta wameikomba mboga yote ilikuwa ni
mboga ya dagaa nilichanganya na nyanya ntole sasa nilikuwaga nawakanya
hawasikii hiyo siku nilishikwa na hasira mara ya kwanza niliwapiga naya pili
hii mara ya tatu kulikuwepo jiko lilikuwa na moto na kulikuwepo na jiko ambalo
nilikuwaga natolea mkaa baada ya kuwapiga nikasogeza hilo jiko ndiyo nikawa
nawababua na kijiko”.amesema Scholastica
Akizungumzia tukio hilo
mtendaji wa kata ya Ibinzamata Victor Kajuna
amesema kuwa taarifa hizo amezipata leo kutoka kwa wananchi waliochukua jukumu
la kuwabeba watoto na kuwapeleka katika ofisi ya afisa mtendaji wa kata
“Leo
majira ya saa nne asubuhi niliwapokea wananchi kutoka mtaa wa Bugwandege
walifika wakiwa wameongozana na mama mmoja pamoja na watoto wake wawili
wakaeleza kuwa baada ya watoto hao kuwaona wanaendelea kuishi bila msaada”.
Diwani wa kata ya
Ibinzamata Mheshimiwa Ezekiel Sabo amekemea kutokea kwa tukio hilo huku
akiwaomba wananchi wa kata hiyo kuacha tabia ya kutoa adhabu kali kwa watoto
wao,kwani kwa kufanya hivyo ni ukatili.
“Taarifa
hii ya watoto kuchomwa moto nimeipokea kwa masikitiko makubwa sana lakini
nakemea swala hili lisijitokeze tena katika kata ya Ibinzamata kwa sababu jamii
ikifikia hapo basi tutakuwa tumefika pabaya sana na niviombe vyombo vya
serikali vifuatilie ili ukatili huu usijirudie tena”.amesema
diwani Sabo
Kwa upande wake afisa
elimu wa kata ya Ibinzamata Mackrine Shija
amewaomba wazazi na walezi kuacha tabia ya kutoa adhabu kubwa kwa watoto.
Msaidizi wa kisheria kutoka Community Edification Organization kata ya Ibinzamata Robert Said amesema kitendo hicho ni ukatili wa kijinsia.
Picha ya Mwanamke Scholastica Peter mwenye umri wa Miaka 28 akiwa katika ofisi ya Mtendaji kata ya Ibinzamata.
Post a Comment