NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KLABU ya Simba imefanikiwa kuichapa
Mbeya City kwa mabao 3-2, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Bejamini
Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Simba Sc ilianza kupata bao la kwanza kupitia
kwa Saidi Ntibazonkiza dakika 11, aliefunga bao zuri na kuhamsha shangwe za
mashabiki waliongia kwenye uwanja huo kushuhudia mchezo huo ambao ulikuwa
wa aina yake.
Ntibazonkiza ameendelea kuuwasha moto ndani ya
uzi wa msimbazi baada ya kufanikiwa kupachika bao la pili dakika 49
ambalo likafanya afikishe mabao tisa kwenye ligi hiyo.
Bao la tatu Simba Sc limefungwa na Pape Sakho
dakika ya 56 ya mchezo, huku mabao ya Mbeya City yakifungwa na
Richardson Ng’ondya dakika ya 13 na bao la pili likifungwa na Juma
Shemvuni dakika ya 78 na mechi kuisha Simba Sc kuondoka na ushindi wa mabao
3-2.
Post a Comment