" TOFFEE UP TOWN ASHEREHEKEA SIKUKUU YAKE YA KUZALIWA NA WANAFUNZI WENYE UHITAJI WA KITUO CHA AGAPE SHINYANGA

TOFFEE UP TOWN ASHEREHEKEA SIKUKUU YAKE YA KUZALIWA NA WANAFUNZI WENYE UHITAJI WA KITUO CHA AGAPE SHINYANGA


Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mdau wa maendeleo wa Mkoa wa Shinyanga Caroline Zacharia Mpemba jina maarufu Toffee up town ametoa msaada wa vitu mbalimbali pamoja na kusherehekea na watoto wenye uhitaji katika shule inayomilikiwa na shirika la Agape Mkoa wa Shinyanga.

Hafla hiyo imefanyika Jumamosi Januari 21,2023 katika ukumbi wa Mazingira Center mjini Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwake Caroline Zacharia Mpemba almaarufu Toffee up town.

Akizungumza katika hafla hiyo Toffee up town amesema ni muhimu jamii kuonyesha upendo kwa watu wenye uhitaji  na kwamba lengo la kutoa msaada huo ni kupunguza changamoto zinazowakabili wanafunzi wanaomilikiwa na shirika la Agape.

Toffee up town pamoja na mambo mengine ametamka rasmi kuwa ameamua kujitolea kuwa balozi wa shirika la Agape ambapo amesema ataendelea kushirikiana nao ili kupunguza changamoto zilizopo na kwamba wanafunzi hao waweze kufikia malengo yao.

"Mimi Caroline Mpemba Jina la Maarufu (Toffee Up Town) Nimefanya Jambo hili kama Mwanamke Mwenye Ushawishi Mkoa wa Shinyanga (Best Female Public Infruencer ) nilipata Tuzo Kupitia Taasisi ya HolySmile Mwaka 2021/2022. Hivyo nimefanya Jambo la Kijamii ili Kurudisha Shukurani kwa Jamii na Tukio hili ni Endelevu nitaendelea kufanya kwenye Jamii katika makundi mbalimbali ya wahitaji".

‘‘Nimeamua kufanya hivi ili kutangaza upendo mjue kwamba kuna watoto wa Agape wapo wanahitaji faraja zetu tuwatie moyo tuwafuata mara kwa mara huko kituoni kwao na kwa kuwapelekea mahitaji, nawapenda sana watoto wangu na nimeamua kujitolea kuwa balozi wenu kila kukicha nitawapambania mimi kama mama kama mlezi na kama mdau wa maendeleo kwa leo nimewaandalia chakula tule pamoja na hili zoezi litakuwa endelevu siyo kwamba nitaishia leo tu’’.amesema Toffee up town

 ‘‘Nawashukuru sana viongozi wangu wa chama na serikali pamoja na wadau mbalimbali kwa kunitia moyo na kunisapoti kwa hali na mali katika shughuli yangu ya kusaidia watoto wenye uhitaji’’.amesema Toffee up town

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la Agape Mkoa wa Shinyanga John Myola  amempongeza  Toffee up town kwa majitoleo hayo huku akieleza kuwa kituo hicho  kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa chakula, vifaa vya shule pamoja na changamoto ya miundombinu.

‘‘Bado tunauhitaji mkubwa kwa watoto wetu, hitaji la kwanza kabisa ni chakula lakini hitaji lingine ni vifaa vya shule yaani matafutari kalamu na sale zingine za shule pamoja na nguo zao binafsi wanahangaika sana lakini pia bado tunahitaji miundominu majengo na vitu vingine vingi vinavyohitajika’’.amesema Myula

‘‘Nawaomba sana awe mama au baba na mtu yoyote mia tano kwetu ni hela kubwa sana tukinunua chumvi itasaidia kwahiyo nawaomba kwa yoyote atakae guswa basi atuletee sisi tutapokea aidha kipekee sana naomba nimshukuru Toffee up town kwa msaada wake huu kwetu utapunguza changamoto tuliyonayo’’.amesema Myula

Naye mkurugenzi wa shirika la Fikra mpya akizungumza kwa niamba ya mashirika Mkoa wa Shinyanga Leah Daud amewasihi wanafunzi wanaosoma katika kituo cha Agape kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao.

Tofee up town ni mdau wa maendeleo wa Mkoa wa Shinyanga alizaliwa Januari 18 ambaye husaidia serikali, chama pamoja na wadau mbalimbali kufanikisha mambo kupitia njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii.

Vitu vilivyotolewa leo kwa ajili ya watoto wenye uhitaji katika kituo cha  Agape ni pamoja na Unga, Sukari, Sabuni, Mchele, Sabuni za unga, Juice maji, Biskuti pamoja na fedha zikiwemo za viongozi na wadau mbalimbali walioguswa kuchangia.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi wa serikali pamoja na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa kikundi cha Shytown VIP na viongozi wa shirika la Lego Liquor Store.


Mdau wa maendeleo wa Mkoa wa Shinyanga Caroline Zacharia Mpemba jina maarufu Toffee up town akizungumza kwenye sherehe yake ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa.

Mkurugenzi wa shirika la Agape Mkoa wa Shinyanga John Myola akizungumza kwenye sherehe ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Toffee up town.

mkurugenzi wa shirika la Fikra mpya akizungumza kwa niamba ya mashirika Mkoa wa Shinyanga Leah Daud akizungumza kwenye sherehe ya kumbukizi ya siku ya  kuzaliwa Toffee up town.

Toffee up town akikabidhi msaada wake kwa mkurugenzi wa shirika la Agape Mkoa wa Shinyanga John Myola.Zoezi la kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali likiendelea katika ukumbi wa mazingira center.Picha ya pamoja kabla ya kuanza zoezi la kula keki ambapo upande wa kushoto ni MC Mama Sabuni.MC Zezema akizungumza kwenye sherehe ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Toffee up townSherehe ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa mdau wa maendeleo Mkoa wa Shinyanga Toffee up town ikiendelea katika ukumbi wa Mazingira center mjini Shinyang









Post a Comment

Previous Post Next Post