" ASKOFU WA JIMBO LA SHINYANGA LIBERATUS SANGU ATAKA WAKRISTO KULINDA IMANI YAO KWA KURITHISHA WATOTO

ASKOFU WA JIMBO LA SHINYANGA LIBERATUS SANGU ATAKA WAKRISTO KULINDA IMANI YAO KWA KURITHISHA WATOTO

 Wakristo wametakiwa kutojiwekea kikwazo katika imani yao, kupitia shughuli za kutafuta riziki zao za kila siku wanazozifanya.

Hayo yamebainishwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, katika Misa ya Jumapili ya Pasaka ambayo imefanyika leo tarehe 09.04.2023 kwenye Kanisa kuu la Mama mwenye Huruma Parokia ya Ngokolo mjini Shimnyanga.
Askofu Sangu amebainisha kuwa, Mkristo hapaswi kutumia muda mwingi kuhangaika na mambo ya kupita, na badala yake anapaswa kuwekeza katika kumtafuta Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kupata uzima wa milele.
Amewataka Wakristo kuhakikisha wanaithamini na kuilinda Imani yao pamoja na kuwarithisha watoto wao imani hiyo kwa kuonesha mfano ndani ya familia kwa kupitia matendo mema yanayompendeza Mwenyezi Mungu.
Askofu Sangu amewaasa Wakatoliki kuwa thabiti katika Imani yao na kuacha tabia ya kutangatanga kwa ajili ya kwenda kutafuta miujiza, ambayo inakwenda kinyume na imani yao.
Amewasisitiza kuendelea kumwamini mwenyezi Mungu na kudumu katika kusali huku wakitambua kuwa, mateso na mahangaiko wanayopitia yanaweza kuondolewa na Mungu mwenyewe na wala siyo kwa miujiza inayotokana na nguvu za binadamu.

Post a Comment

Previous Post Next Post