" SERIKALI YA MKOA WA SHINYANGA KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WA DINI

SERIKALI YA MKOA WA SHINYANGA KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WA DINI

 Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amesema serikali itaendelea kuthamini na kudumisha ushirikiano uliopo kati yake na taasisi za dini.

Mndeme ametoa kauli hiyo wakati akitoa salamu za Serikali, katika Misa ya mkesha wa Pasaka ambayo imefanyika katika Kanisa kuu la Mama mwenye huruma Parokia ya Ngokolo mjini Shinyanga.
Amesema taasisi za dini ikiwemo Kanisa Katoliki zimekuwa na mchango mkubwa katika kuisaidia Serikali kutoa huduma mbalimbali za kijamii na hasa kwenye sekta za afya, elimu na kilimo.
Pia amewashukuru viongozi wa Kanisa Katoliki na dini nyingine kwa mchango wao mkubwa katika kudumisha hali ya amani na mshikamano ndani ya taifa, kupitia sala na dua wanazozitoa.
Kwa upande wake Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, ameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali kupitia huduma mbalimbali za kijamii zinazotolewa na Kanisa, kwa ajili ya ustawi wa watu wa Shinyanga na maendeleo ya taifa.
Askofu Sangu ametumia nafasi hiyo kuwaasa Watanzania kuendelea kuilinda tunu ya amani ambayo Mwenyezi Mungu amewajalia, kwani baadhi ya mataifa yaliyoko kwenye migogoro ya mara kwa mara yanatamani kuiona Tanzania ikiingia katika hali hiyo.


Post a Comment

Previous Post Next Post