Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, ametuma salaam za Pasaka kwa waamini na watu wote, huku akisisitiza kudhibitiwa kwa vitendo vya ushoga na usagaji ndani ya jamii.
Ametoa wito kwa viongozi wenzake wa dini na viongozi wa Serikali kupitia dhamama waliyonayo, kuungana kwa pamoja kupambana na janga hilo, ambalo amelitaja kuwa limefichika katika kile kinachoitwa misaada kwa maendeleo na haki za bibadamu.
Amemuomba rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na wandamizi wake wakiongozwa na dhamiri njema ya kuliongoza taifa katika misingi ya haki, upendo na amani, kutosahau kuwakumbusha watanzania kama mama, yale yanayofaa na kupiga vita yote yanayoelekea kuliingiza taifa katika unajisi wa ushoga na usagaji.
Amewasihi wasimamizi na waandaaji wa maudhui katika vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii, kutotoa nafasi kwa watu wanaojihusha masuala ya ushoga na usagaji, na badala yake wajikite katika kuandaa madhui ya kuijenga na kuisaidia jamii.
Askofu Sangu pia amewakumbusha Watanzania kutochoka kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kwamba, juhudi hizo ziende mbali zaidi kwa kupinga vitendo vyote vya ukatili dhidi ya binadamu.
Wakati huohuo Askofu Sangu ameipongeza Serikali kupitia rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa juhudi inazozifanya katika uhifadhi wa Mazingira.
(BONYEZA LINK HAPO CHINI KUONA VIDEO)
Post a Comment