
JESHI la polisi mkoa wa Iringa linamshikilia Amani Martin maarufu kwa jina la Kasisi (47) mkazi wa Nzihi wilaya ya Iringa ambae pia ni kiongozi wa dini kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi saba kwa madai ya kudanganywa na shetani.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Allan Bukumbi aliwaeleza wanahabari leo ofisini kwake kuwa tukio hilo lilitokea Machi 28 majira ya saa saba mchana na kumsababishia maumivu makali sehemu za haja kubwa .
Alisema kuwa Kasisi ambae ni mkulima wa Kijiji cha Nzihi alidai kuwa alifanya tukio hilo baada ya kudanganywa na shetani na kuwa anajutia kutenda unyama huo kwa mwanae .
Alisema kuwa mama wa mtoto huyo Magreth Kaguo (29) ndie ambae alibaini mtoto wake huyo kulawitiwa na kuwa mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani wakati wowote .
Katika tukio jingine jeshi la polisi linamshikilia mtuhumiwa mmoja jina limehifadhiwa kutokana na sababu za kiuchunguzi ambae anatuhumiwa kukodisha silaha kwa wahalifu .
Kamanda Bukumbi alisema kuwa mtuhumiwa huyo mkazi wa eneo la Kihesa Kilimani Manispaa ya Iringa alikamatwa April 3 majira ya 11 jioni baada ya taarifa fichi kutoka kwa wasamaria wema kuhusiana na biashara isiyo rasmi ya ukodishaji silaha mbili aina ya shotgun yenye namba za usajili TZ CAR 6271 na Rifle yenye namba za usajili CAR 48081 ambayo imepelekwa kikosi cha mizinga mkoa wa Morogoro kwa ajili ya matengenezo ,kuwa kupitia mwanya huo amekua akijipatia fedha kwa njia ya kukodisha silaha na risasi kwa kiasi cha shilingi 100,000 kwa tukio .
“ mtuhumiwa huyo amekuwa akikodisha silaha hizo kwa watu mbali mbali kitu ambacho ni kinyume na utaratibu wa matumizi ya silaha na sheria za nchi .
Kamanda Bukumbi alisema tukio jingine ni lile lililotokea April 4 mwaka huu eneo la Mwangata A kata ya Mwangata Manispaa ya Iringa kwa jeshi hilo kufanya msako na kufanikiwa kukamata silaha aina ya Pistol Rami yenye namba za usajili A935520 pamoja na risasi zake 10 ndani ya Magazine ambayo ilisalimishwa karibu na nyumba ya mwenyekiti wa mtaa wa Mwangata A Batista Kisonga baada ya mtuhumiwa Rashid Nyomolelo kuiba kutoka kwa Joseph Philipo Lukonde (44) mkazi wa Nkuhungu mkoani Dodoma mtuhumiwa bado anatafutwa .
Wakati huo huo Julius Mlwale(36) mkulima mkazi wa Kijiji cha Mgama wilaya ya Iringa amekamatwa na jeshi la polisi mkoani hapa akiwa na silaha aina ya Shortgun fupi iliyotengenezwa kienyeji isiyokuwa nan amba za usajili maarufu kama Kipalupalu akiwa ameificha ardhini ambayo alikuwa akiitumiwa kwa matukio ya uhalifu.
Kuwa mtuhumiwa huyo amedai kuwa amekuwa akiitumia silaha hiyo katika matukio mbali mbali ya uhalifu na alikamatwa April 5 majira ya saa 6 mchana katika Kijiji hicho na kuwa mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati wowote .
Wakati huo huo jeshi la polisi la Polisi mkoa wa Iringa limeanza uchunguzi wa kuhoji taasisi zinazotuhumiwa kujihusisha na uhamasishaji wa vitendo vya ushoga na ndoa za jinsia moja.
Post a Comment