
NA HADIJA OMARY,LINDI.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi zainab Telak leo April 11/2023 amepokea mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Mtwara kutoka kwa Mkuu wa mkoa huo kanali Ahmed Abbas.
Makabidiano hayo yamefanika katika kata ya Nyangao halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi ambayo yaliudhuliwa na viongozi mbali mbali wa Mkoa na Wilaya pamoja na wananchi wa maeneo hayo na maeneo jirani.
Mwenge huo wa uhuru utanza kukimbizwa mbio zake Mkoa Lindi leo April 11 /2023 katika Halmashauri ya Mtama kisha Ruangwa, Manispaa ya Lindi , Kilwa, Liwale na kimalizia Halmashauri ya Nachingwa mnamo April 16 /2023.

Akipokea Mwenge huo Bi Zainabu Tellack alisema kuwa mwenge huo wa uhuru utakimbia katika wilaya tano za Mkoa huo kwa umbali wa kilometa 1050 na utatembelea, utazindua na kuweka mawe yamsingi Miradi ya Maendeleo 61 yenye thamani ya Shilingi bilioni 51.5
Bi. Zainab aliongeza kuwa kati ya miradi hiyo 61 miradi 15 itawekwa mawe ya msingi ,10 itazinduliwa na miradi 35 itakaguliwa na kuonwa ambapa mchango wa Serikali kuu ikiwa ni shilling milioni 50.6 Halmashauri milioni 353 nguvu za Wananchi milioni 65.2 na wadau wa maendeleo ni milioni 466.8.
Kwa upande wake Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Abdallah Shaib Kaim aliwataadhalisha viongozi wa Mkoa na Wilaya kuwepo na nyaraka zote muhimu katika miradi husika ambayo itatembelewa na Mwenge huo ili waweze kuzipitia kwa kina na kujidhisha.
“Naomba niwakumbushe viongozi wangu wa Mkoa wa Lindi katika miradi yote tutakayoitembelea huko Wilayani kwenu naomba nyaraka zote zinazohusika ziwepo na tuzipate asubuhi Mapema kabla hatujaanza kutembelea miradi yenyewe hii itatupa sisi urahisi wa kuzipitia taarifa mapema” alisema kaimu
Kaulimbiu ya mwenge wa uhuru mwaka 2023 inasema " Tunza mazingira okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai kwa uchumi wa Taifa"



Post a Comment