Jamii imetakiwa kusimama kwa pamoja katika kutetea haki za watoto yatima na wanawake wajane kutokana na dhuluma mbalimbali wanazofanyiwa.
Rai hiyo imetolewa na Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, wakati akiwahubiria waamini katika ibada ya Ijumaa kuu, iliyofanyika leo tarehe 07.04.2023, katika Kanisa kuu la Mama mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga.
Ameeleza kusikitishwa kwake na hali ilivyo hivi sasa, ambapo baadhi ya ndugu wamefikia hatua ya kuiba hata fedha za rambirambi ambazo zinatolewa kwa ajili ya kuisaidia familia ya marehemu.
Askofu Sangu pia ametoa wito kwa jamii kuwajali, kuwafariji na kuwasaidia watu wenye shida mbalimbali, ikiwemo yatima, wafungwa na wagonjwa.
Post a Comment