Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mchungaji Charles Lugembe wa Kanisa la AICT
Kambarage mjini Shinyanga amewaasa wakristo kutokatishwa tamaa na changamoto
mbalimbali zinazojitokeza katika maisha yao,ikiwemo mateso yanayosababishwa na
magonjwa na sababu nyingine.
Ameyasema hayo leo wakati akihubiri katika
ibada ya Jumapili iliyofanyika katika Kanisa la AICT Kambarage mjini Shinyanga
ambapo amewataka waumini hao kuwa wavumilivu na kutokatishwa tamaa na
changamoto zozote zinazojitokeza mbele yao.
Amewaasa waaumini hao kuendelea kumcha Mungu
na kusimama katika Imani kama njia ya kuufikia ufalume wa Mungu.
Mchungaji Lugembe ameeleza kuwa zipo njia
mbalimbali zinazomuwezesha mkristo kuwasiliana na Mungu ikiwemo kupitia
mafundisho ya Kanisa.
Kwa upande wao waumini wa Kanisa hilo wamesema kupitia ibada mbalimbali wanazoshiriki Kanisani hapo imekuwa ikiwasaidia kuwa na Imani thabiti lakini pia kupata Baraka za Mungu.
Post a Comment