Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora, Hassan Wakasuvi enzi za uhai wake.
Waziri mkuu Kassim
Majaliwa anatarajiwa kuongoza viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo wa vyama
vya siasa, serikali na wananchi wakati wa mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa
chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Tabora na mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa
Hassan Wakasuvi
Akitoa taarifa ya
ratiba ya mazishi hayo katibu wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Tabora Elias
Mpanda amesema kuwa mazishi hayo yatafanyika kesho katika kijiji cha Mabama
ambako ndiko nyumbani kwa marehemu nje kidogo ya Manispaa ya Tabora.
Kwa mujibu wa mganga
mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya Kitete Mkoani Tabora Dkt. Marco Waziri kifo
cha ghafla cha Hassan Wakasuvi kilichotokea jana mchana kimetokana na shambulio
la moyo.
Chama Cha Mapiduzi kikiongozwa na Mwenyekiti wake na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan , kimepokea kwa masikitiko makubwa na kutoa salamu za rambirambi na pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na wanachama wote kufuatia kifo cha Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Hayati. Hassan Wakasuvi.
Post a Comment