HomeMICHEZO AZIZI KI, DIARA NA MUSONDA WAITWA TIMU ZA TAIFA. Misalaba March 16, 2024 0 Na Elisha Petro, ShinyangaKlabu ya Yanga imethibitisha taarifa ya wachezaji wake watatu wa kigeni kuitwa katika timu zao za taifa baada ya nyota wengine watano kuitwa kujiunga na timu ya taifa ya Tanzania (Taifa stars).Nyota hao ni Stephani Azizi Ki ni nyota aliyeitwa kujiunga na kikosi Cha Burkina Faso, Kennedy Musonda akiitwa kujiunga na kikosi Cha Zambia na nyota wa mwisho ni Djigui Diarra aliyeitwa kujiunga na kikosi cha timu ya taifa ya Mali.Nyota wengine walioitwa kujiunga na timu ya taifa ya Tanzania (Taifa stars) ambao ni golikipa Aboutwaleeb Mshery, mabeki wawili Ibrahim Bacca na Bakari Mwamnyeto, kiungo Mudathir Yahya na mshambuliaji Clement Mzize.Nyota hao ni miongoni mwa wachezaji watakaokuwa sehemu ya kikosi dhidi ya wenyeji wao Azam FC. Kesho March 17, 2023 klabu ya Yanga itashuka dimbani kuwakabiri wenyeji wa mchezo huo klabu ya Azam FC katika uwanja wa Azam Complex. You Might Like View all
Post a Comment