Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha.
Na Moshi Ndugulile
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha amesema vijana ni nguvu kazi ya Taifa hivyo wana wajibu mkubwa wa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kuchangia katika ustawi na Maendeleo ya Mkoa na Taifa
Ametoa kauli hiyo leo kwenye hafla ya kujitambulisha iliyofanyika kwenye hotel ya karena Mjini Shinyanga,ambayo imetanguliwa na makabidhiano ya ofisi, ikiwa ni siku chache baada ya kuapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
RC Macha amewataka vijana kujikita katika shughuli za kuwaletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kutumia vyema fursa zinazojitokeza mbele yao kuleta tija na ufanisi,badala ya kujihusisha na makundi mabaya ikiwemo kucheza michezo ya kubahatisha (kamali)
Amesema serikali itaendelea kuwahakikisha kuwepo kwa mazingira ya Amani,usalama na upatikanaji wa huduma bora na stahiki za kijamii,uzingatiwaji wa misingi ya utawala bora,haki na utu kwa wananchi wote wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu huyo wa Mkoa ameonya tabia ya baadhi ya watendaji kujihusisha na masuala ya kisiasa ambapo amesema kwa kufanya hivyo ni kubeba majukumu yasiyowahusu,na badala yake amewataka kuwatumikia wananchi kwa uadilifu.
Amesisitiza viongozi na watendaji wa serikali kufanya kazi kwa umoja,mshikamano na ushirikiano wa dhati mazingira ambayo yatasaidia kuwaepusha na mianya ya chuki,na migogoro
Anamringi Macha amewataka viongozi na watendaji kutoka ofisi na kwenda kusikiliza kero za wananchi zikiwemo zile za migogoro ya ardhi
Akizungumza katika hafla hiyo naibu katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Bi Christina Mndeme ameomba viongozi wa Dini, serikali,vyama vya Sasa, taasisi za serikali na sekta binafsi, wadau wote wa Maendeleo na wananchi kumpatia ushirikiano Mkuu huyo wa Mkoa ili kuendelea kuchochea ukuaji wa Uchumi na Maendeleo.
Mndeme amewaomba wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kushiriki vema kwenye ajenda ya kitaifa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kuendelea
kutunza mazingira.
Anamringi Macha anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akichukua
nafasi ya Christina Mndeme ambaye amekuwa naibu katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa
Rais mazingira na Muungano,na kwamba kabla ya uteuzi huo alikuwa naibu katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Bi. Odilia Batimayo.
Christina Mndeme Naibu katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya ofisi baina ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Naibu katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya ofisi baina ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Naibu katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.
Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Janeth Magomi na Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Shinyanga Frank Mahimbali.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo.
Shekh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya ofisi baina ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Naibu katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.
Mganga Mfawidhi Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. Luzila John.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya ofisi baina ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Naibu katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga Bwana Faustine Mdessa
Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya ofisi baina ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Naibu katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.
Christina Mndeme Naibu katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akipokea zawadi kutoka kwa watumishi ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Christina Mndeme Naibu katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akipokea zawadi kutoka kwa watumishi ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akipokea zawadi kutoka kwa watumishi ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Christina Mndeme Naibu katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akipokea zawadi kutoka kwa kamanda wa jeshi la Polisi kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Janeth Magomi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akipokea zawadi kutoka kwa kamanda wa jeshi la Polisi kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Janeth Magomi.
Christina Mndeme Naibu katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akipokea zawadi
Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya ofisi baina ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Naibu katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.
Picha na Mapuli Kitina Misalaba, Shinyanga
Post a Comment