Na Swalehe Magesa,Misalaba Media - Bunda, Mara.
- Wakulima wa zao la pamba Bunda wamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia mashine ya umwagiliaji Boom splayaer pump.
- Bodi ya Pamba yatoa elimu kwa wakulima jinsi ya kutumia mashine ya umwagiliaji ya Boom splayaer pump.
Wakizungumza na Jambo Digital Tv wakulima wa zao la pamba wilayani Bunda ( Bunda Dc ) mkoani Mara, wameishukuru Serikali kwa kuwapatia mashine ya Boom splayaer pump ambayo imekuwa mkombozi kwenye umwagiliaji wa mashamba,hata hivyo wameiomba Serikali kuongeza zaidi ili iwe rahisi kumwagilia mashamba mengi zaidi.

"Angalia kwasasa iko moja kwa kijiji chote ambacho tuna heka mia tano za zao hilo, mashine aitoshi leo amepiga huyu hapa, kesho anaitaji mwingine aitumie, siku moja kunaweza kuwa na uitaji zaidi ya watu watano kwa hiyo tunaomba Serikali iweze kuongeza zaidi,"Patrick Kabati - Mkulima wa pamba kijiji cha Mwiseni.
Kwa upande wake Afisa Kilimo kijiji cha Mwiseni kutoka Bodi ya Pamba Shija Seleman amesema, pump hiyo imekuwa ikirahisisha katika umwagiliaji,ukilinganisha na pump za kubeba mgongoni ambazo zilikuwa na changamoto ya kuwachosha wakulima pia waliweza kumwagilia mashamba machache.
Nae mkulima wa zao la pamba katika kijiji cha Igundu kata ya Bulendabufwe wilayani humo Mkama Nyaonge amesema,mashine hiyo imekuwa aina usumbufu katika suala la umwagiliaji tofauti na ile ya kubeba mgongoni ambayo ilikuwa mzigo kwake.
" Chombo hiki ni faraja kubwa kwa wakulima kinasaidia unafanya kazi kwa wepesi aina usumbufu shida yake ni pale mafuta ya petrol yanapoisha lakini suala la umwagiliaji liko vizuri sana,"Mkama Nyaonge - mkulima wa zao la pamba katika kijiji cha Igundu kata ya Bulendabufwe.
"Utaratibu wa kutoa mashine hiyo tumekuwa tukitoa kipaumbele kwa wakulima wenye mashamba makubwa na imesaidia matumizi sahihi ya vipimo kwenye upandaji wa mbegu kwa kuacha nafasi ya kupitisha mashine kwa ajili ya umwagilia wa viwatilifu," Simeo Nkwabi - Afisa kilimo kijiji cha cha Igundu kata ya Bulendabufwe.
Post a Comment