" WATOA HUDUMA YA MAJI NGAZI YA JAMII WAPATIWA PIKIPIKI

WATOA HUDUMA YA MAJI NGAZI YA JAMII WAPATIWA PIKIPIKI

Na Lucas Raphael -Misalaba Media, Tabora 

Mkuu wa wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Naitapwaki Tukai amekabidhi pikipiki 24 kwa watoa huduma ya maji ngazi ya jamii(CBWSOs) zikiwa na thamani ya shilingi milioni 67.

Alikabidhi Pikipiki hizo  zilizotolewa na wakala ya maji na usafi wa mazingira vijjini RUWASA na kusisitiza wazitumia Pikipiki hizo zitumika kwa kazi iliyokusudiwa kwa kutoa huduma kwa  jamii inayoitaji huduma ya maji vijijini .

Tukai  alisema kwamba kupatikana kwa vitendea kazi hivyo vitasaidia kuweza kuwafikia wananchi kwa wakati mara wanapoitaji kupatiwa huduma bora ya maji na  kuhakikisha huduma ya maji inaboreka maeneo mbalimbali ya vijiji.

Aliiendelea kusema katika utekelzaji wa  ilani ya chama cha mapinduzi inayolekeza kufikia mwaka 2025 maji vijiji kuweza kufikia lengo la asilimia 85 na mijini lifikie asilimia 95 .

Alisema kwa kutekeleza ilani hiyo halmashauri ya wilaya ya nzega vijijini  imefikia asilimia 86 mijini lengo limevukwa na kufikia asilimia 98.

Tukai aliendelea kueleza kuwa ili kuweza kufikia malengo hayo nilazima kila mtoa huduma ngazi ya jamii anapaswa kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakiksha wananchi wanapata huduma bora ya maji.

Awali kaimu meneja wakala ya maji na usafi wa mazingira vijjini RUWASA katika  halmashauri ya wilaya ya Nzega Mhandisi Faustine Makoka alimweleza mkuu huyo wa wilaya kuwa kuwapatia vitendea kazi watoa huduma ngazi ya jamii lengo ni kuwafikia  wananchi kwa wakati na kutoa huduma.

Hata hivyo alisema kwamba licha ya pikipiki hizo pia wametenga kiasi cha shilingi milioni 480  kwa ajili ya ujenzi wa ofisi 6 za vyombo vya watumiaji maji ngazi ya jamii (CBWSOs) .

Alisema ofisi  hizo ni  Jumuia za Umwai ,Ubuki, Bukau ,Mwaisaka ,ubinga na jumuia ya Kinamwaka, .

Mhandisi Makoka aliishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kusaidia huduma ya  maji katika wilaya ya nzega mkoani hapa. kaimu meneja wakala ya maji na usafi wa mazingira vijjini RUWASA katika  halmashauri ya wilaya ya Nzega Mhandisi Faustine Makoka akitoa maelezo mafupi wakati wa kukabidhi  Pikipiki  watoa huduma ya maji ngazi ya jamii(CBWSOs).

 

Post a Comment

Previous Post Next Post