
Mwenyekiti wa kampeni
ya shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga Bi. Nabila Kisendi amewataka wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuacha
kuwatendea ukatili watoto ikiwemo kuwaadhibu kupita kiasi.
Ametoa rai hiyo baada
ya kutembelea familia ya mtoto anayesadikiwa kufanyiwa ukatili kwa kuadhibiwa
vikali na baba yake mdogo ambapo mtoto huyo anasoma katika shule ya msingi
Itogwaholo kata ya Isaka Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga.
Imeelezwa kuwa mtoto
huyo aliyesadikiwa kufanyiwa ukatili na baba yake mdogo alikuwa anaamshwa saa
kumi na moja alfajili kufanya kazi hapo nyumbani na kusababisha kuwa anachelewa
shuleni kila siku.
Pia imeelezwa kuwa
mwanafunzi huyo alikuwa akisinzia darasani mara kwa mara ambapo walimu wake
katika Shule ya msingi Itogwaholo kata ya Isaka walizungumza naye na kubaini changamoto
anazopitia na kwamba walimwita huyo mlezi baba yake mdogo nakumonya.
Baada ya kuonywa mlezi
huyo bado aliendelea kumfanyia ukatili ikiwemo kumuadhibu vikali ambapo
mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Mwalimu Nabila Kisendi alipigiwa simu
ambapo alienda kumshuhudia mtoto huyo akiwa ameongozana na viongozi wengine
mbalimbali akiwemo afisa maendeleo ya jamii wa kata ya Isaka na kwamba tayari
mtuhumiwa huyo amefikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa ajili ya hatua zaidi.
Mwenyekiti wa SMAUJATA
Mkoa wa Shinyanga Bi. Nabila Kisendi ametumia nafasi hiyo kuwasisitiza
wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuacha kuwafanyia ukatili watoto ikiwemo kuwaadhibu kupita
kiasi hali hiyo ni ukatili wa kimwili na huathiri kisaikorojia.
SMAUJATA ni kampeni ya kupinga ukatili ambayo inatekeleza majukumu yake chni ya wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum ambapo viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa shinyanga wameendelea kuibua na kutoa elimu ya ukatili kwenye jamii na taasisi mbalimbali.
Post a Comment