Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu kesho tarehe 12.04.2024, atafanya kumbukumbu ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kuwa Askofu wa nne wa Jimbo la Shinyanga, miaka 9 iliyopita.
Askofu Sangu aliwekwa wakfu na kusimikwa kuwa Askofu wa nne wa Jimbo la Shinyanga mnamo tarehe 12.04.2015, na Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo kuu la Dar es salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, ambaye wakati huo alikuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dar es salaam, akisaidiwa na Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es salaam Mhashamu Jude Thedeus Ruwaich, ambaye wakati huo alikuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Mwanza na Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Tabora Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa, ambaye wakati huo alikuwa Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu.
Alipokelewa Jimboni Shinyanga akitokea Jimbo la Sumbawanga siku kama ya leo tarehe 11.04.2015, katika eneo la Mto Manonga Parokia ya Busanda mpakani mwa Jimbo la Shinyanga na Jimbo kuu la Tabora.
Post a Comment